Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (MB) akihutubia wakati
wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu
Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika
ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Baadhi
ya Wakufunzi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (hayupo pichani)
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa
Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika
ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungua rasmi
Mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema
uliopo Morogoro mjini. (Picha zote na Veronica Kazimoto – Morogoro)
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo
akitoa maelezo ya utangulizi katika ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya
Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014
yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
………………………………………………………………………………
Ukosefu
wa Ajira umekuwa ni changamoto kubwa kwa sasa duniani kote ambapo
ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu hali ya
ajira duniani, inaonesha kuwa takribani watu milioni 197 sawa na
asilimia 5.9 ya nguvu kazi duniani hawana kazi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga
wakati akifungua Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema
uliopo Morogoro mjini.
Dkt.
Mahanga amesema kati ya watu 197 ambao hawana kazi vijana ni milioni
73.8 sawa asilimia 12.6 ambayo ni nguvukazi inayopaswa kutumika ipasavyo
kwa kuwa kuna mahusiano makubwa kati ya ukuaji wa tija na matumizi ya
nguvukazi.
Ameongeza
kuwa, kutokana na changamoto hiyo ya ajira, ni muhimu kufanya Utafiti
wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya kazi ili kuisaidia Serikali kufuatilia
mwenendo wa mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira.
Mahanga
amefafanua kuwa utafiti huu utasaidia pia kuboresha sera na program
mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango
ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka
2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.
Kwa
upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Ephraim Kwesigabo amesema lengo kuu la Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi ni kukusanya takwimu zinazohusu hali ya soko la ajira
nchini.
Kwesigabo
amesisitiza kuwa utafiti huo utawezesha kupata viashiria vinavyohusu
ajira na ukosefu wa ajira kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii
na hivyo kuisaidia Serikali kuboresha sera ya kukuza ajira nchini.
Mafunzo
hayo ya wiki mbili yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo
jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaendelea kupewa
mafunzo juu ya Utafiti huo wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi
utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka 2014.
Na Kamanda wa Matukio