Hivyo ndivyo maiti ilivyoPICHA ZOTE NA MTANDA BLOG
safirishwa kutoka Tundama mpaka Morogoro baada ya kukamatwa.
Askari kanzu akiichunguza maito muda mfupi kabla ya kutemshwa.
maiti ya marehemu Khalid Kitala ikishushwa kutoka kwenye gari tayari kwa uchunguzi katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti
wakiandaa maiti muda mfupi kabla ya kuipasua tumbo na kutoa kete 17
zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Simu tano za wathumiwa zikiwa katika
kituo kikuu cha polisi na kete 24 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya
kulevya, kete 17 zilitolewa katika tumbo la marehemu baada ya kulipasua
na kete sana zilikutwa katika gari ya watuhumiwa husika, Hizo kete
zinazofanana na rangi ya njano ndizo zilizotolewa tumboni mwa marehemu
Kete saba ndizo zilizokutwa katika gari baada ya kupekuliwa.
Kete saba ndizo zilizokutwa katika gari baada ya kupekuliwa.
Hii ndiyo gari iliyobeba maiti kutoka Tunduma kabla ya kukamatwa Mikumi Morogoro wakati ikielekea jijini Dar es Salaam na maiti.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
mkoa wa Morogoro akihesabu kete, muda mfupi kabla ya Kamanda Faustine
Shilogile kuongea na waandishi wa habari juu ya tukio hilo.
Huyu ndiye Kamanda Faustine Shilogile
akiwaonyesha moja ya kete iliyotolewa tumboni mwa marehemu Khalid Kitala
baada ya kusua tumbo kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo.
MAITI ILIYOKUTWA NA KETE 17 ZA MADAWA YA KULEVYA YAKABIDHIWA KWA FAMILIA
LILIAN LUCAS, Morogoro.
MWILI wa aliyekuwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam, Khalid Kitara (47) uliokutwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni heroini, umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.
MWILI wa aliyekuwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam, Khalid Kitara (47) uliokutwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni heroini, umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kwamba baada ya
kufanyika kwa uchunguzi huo wameamua kukabidhi mwili huo huku
wakiendelea na upelelezi kubaini mtandao unaohusika na tukio hilo.
Alisema jeshi hilo bado linaendelea kuwashikilia
watuhumiwa watatu, ambao ni madereva wawili waliokuwa wakipokezana
kuendesha gari hilo ambao aliwataja kuwa ni Teddy Sichilima (27), mkazi
wa Tunduma Mbeya, Lucas Atubonekisye (32), mkazi wa Mtaa wa Songea,
Tunduma na aliyekutwa na mwili wa Marehemu, Jumbe Mbano (36),
mfanyabiashara na mkazi wa Kariakoo. Alisema watu hao watafikishwa
mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
Alitoa wito kwa jamii kuendelea kuwafichua
wahalifu ili sheria ichukue mkondo wake huku akisisitiza azma ya polisi
kupambana kuhakikisha linatokomeza biashara ya dawa ya kulevya ambazo
kwa sasa uuzaji wa dawa hizo umeonekana kuzagaa nchini.
MBARAONI WAKIDAIWA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA WAKITUMIA MAITI.
POLISI mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha maiti inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.
MBARAONI WAKIDAIWA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA WAKITUMIA MAITI.
Watuhumiwa
Teddy Esco Sichirima (27) mkazi wa mtaa wa Mwaka-Tunduma, Lucas
Atubonekisye Swila (32) mkazi wa mtaa wa Sogea Mbeya na Jumbe Hamad
Mbano mfanyabiashara mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ndugu wa
marehemu Khalid Abdul Kitala (47) wakiwa chini ya ulinzi eneo la chumba
cha kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
POLISI mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha maiti inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.
Taarifa za vyanzo vya kuaminika, zilisema watuhumiwa walikuwa wakitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam.
Habari zilisema walipofika Mikumi, wilayani Kilosa gari hilo lilisimamishwa na trafiki lakini dereva alikataa kusimamama.
Imeelezwa kuwa kitendo hicho kiliwapa mashaka trafiki na kulazimika kulifuatilia gari hilo lililokuwa katika mwendo mkali.
Kwa mujibu wa habari hizo baadaye askari waliamua kufyatua risasi hewani, kitendo kilichowafanya watu hao kusimama.
Baada ya kusimama, askari walianza kuwahoji watu hao kuhusu hatua yao ya kukataa kusimama.
Inasemekana katika majibu yake mmoja wa watuhumiwa, alidai kuwa wanasafirisha maiti ya baba mkwe wake.
Ilidaiwa kuwa watu hao walikuwa wakisafiri na mtu
huyo kabla hajafa kwenda Zambia, lakini walipofika Tunduma, alifariki
dunia na baadaye watu hao waliamua kuirejesha maiti yake jijini Dar
es Salaam kwa maziko.
Askari wa upelelezi wa Kituo Kikuu cha Polisi cha
mjini Morogoro, walionekana wakitoa kete za dawa ya kulevya kutoka
kwenye buti la gari.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Litha Lyamuya alisema mwili wa mwanaume umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukukutwa na vitu vinavyofanana na pipi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Litha Lyamuya alisema mwili wa mwanaume umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukukutwa na vitu vinavyofanana na pipi.
NA LILIAN LUCAS, Morogoro.
Kwa hisani ya Mtanda Blog