TUME YA KATIBA KUMKABIDHI MHE. RAIS RIPOTI NA RASIMU YA KATIBA JUMATATU DISEMBA 30, 2013 SAA 6:00 MCHANA


                                       JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
 
Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
 
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na rasimu ya Katiba.
 
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, anuani za posta, tovuti (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).
 
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
Disemba 27, 2013.
 


Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (0) 757 50080j0,
Website: www.katiba.go.tz