SERIKALI YATANGAZA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA
Jumla
ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza
darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari
katika shule za Serikali.
Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.
Akitangaza
idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu
Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na
tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini
kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hadi ifikapo
machi mwaka mwakani.
Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.
Amesema
idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana
na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya
madarasa 412.
Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia