Kuwait City
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema leo kuwa ana matumaini kura ya maoni inayofanyika nchini Misri kuidhinisha katiba mpya , itafanyika kwa uwazi na kuaminika.
Naibu msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Marie Harf amesema kuwa bila kujali matokeo ya kura hiyo ya maoni ni muhimu kwa serikali ya mpito kuweka mazingira bora kwa ajili ya vyama vya kijamii. Marekani ilizuwia misaada yake, ambayo sehemu kubwa inakwenda katika jeshi, baada ya kuangushwa kwa utawala wa rais Mohammed Mursi. Marekani imesisitiza kuwa serikali iliyowekwa na jeshi inalazimika kuirejesha nchi hiyo katika njia ya kidemokrasia.
Na DW.DE