Madaktari na familia ya waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon
wanashauriana namna ya kuendelea na matibabu ya mwanasiasa huyo
mwenye umri wa miaka 85.
Sharon amepoteza fahamu kwa miaka minane,
na hali yake imeendelea kuwa mbaya katika siku za karibuni.
Vyombo vya
habari vya Israel vimeripoti kuwa anaugua maradhi ya figo na madaktari
wamesema wanahofia maisha yake.
Sharon aipatwa na ugonjwa wa kiharusi
na kuvuja damu kwenye ubongo mnamo Januari 4 mwaka wa 2006, wakati
akiendelea na kampeni za uchaguzi ambao alitarajiwa kushinda.
Alikuwa
Waziri Mkuu wa Israel kuanzia mwaka wa 2001 hadi mwaka wa 2006.
Aliunga
mkono ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi katika maeneo ya
wapalestina yanayokaliwa na Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)