Showing posts with label Israel. Show all posts
Showing posts with label Israel. Show all posts

Israel:Wanajeshi wetu hawaendi ICC

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa hatakubali wanajeshi wake kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.
Alikuwa akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri tangu Palestina ilipotuma ombi la kujiunga na mahakama ya ICC ambayo wana imani itaifungulia mashtaka Israel kwa madai ya uhalifu wa kivita katika maeneo inayokalia.
Israel imesema kuwa wanajeshi wake hawatakwenda mbele ya mahakama ya IIC kujibu mashtaka
Bwana Netanyahu ameishtumu Palestina kwa kutumia njia ya mapambano.
Israel imezuia kitita cha dola millioni 125 ufadhili wa fedha za kila mwezi kwa Palestina kama kodi inayochukua kwa niaba yake kama makubaliano ya mkataba wa amani.
Hatahivyo Palestina imepinga hatua hiyo ikitaja kama adhabu dhidi yake.
Israel yasema imeidungua ndege ya kivita ya Syria

Israel yasema imeidungua ndege ya kivita ya Syria


Jeshi la Israel limesema limeiangusha ndege ya kivita ya Syria katika milima ya Golan, ikisema ilikuwa imevuka mpaka wa usitishaji mapigano katika eneo linalokaliwa na Israel.  Hili ni tukio kubwa zaidi kutokea katika eneo hilo tangu kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria mwaka wa 2011.
Image result for Israel Pix 

Taarifa iliotolewa na jeshi la Israel ambayo haikuwa na maelezo zaidi ilisema ndege hiyo iliyoingia eneo la Israel ilifanikiwa kudunguliwa muda mchache kwa mfumo wa kujilinda wa angani karibu na mpaka wa Syria. Kudunguliwa kwa ndege hiyo kunakuja wiki tatu baada ya Israel kuiangusha ndege nyengine isokuwa na rubani iliokuwa katika anga ya milima ya Golan wakati mapigano yakipamba moto upande wa Syria, ambapo eneo kubwa linashikiliwa na waasi wanaopigana kuuangusha utawala wa Bashar Al Assad. Syria imethibitisha kuangushwa kwa ndege yake ya kivita na kukielezea kitendo hicho kuwa cha uchokozi.

HIVI NDIVYO WAZIRI WA ZAMANI WA ISRAEL "ARIEL SHARON" ALIVYOZIKWA LEO




Ibaada maalum ya aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel Ariel Sharon imefanyika nje ya majengo ya bunge la Israel.
Bwana Sharon atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa taifa la Israel lakini pia alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa jasiri aliyechukiwa na wapalestina wengi.








Waliohutubia umati,wamemtaja Sharon kama mtu aliyejitolea kuhakikisha kuna usalama kwa watu wake.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alisema kuwa Sharon alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa wayahudi na ambaye atakumbukwa zaidi ya wote.
Licha ya sifa hizo Bwana Sharon anachukiwa sana na waarabu hasa wapalestina kwa dhuluma alizowatendea chini ya utawala wake.


Kiongozi huyo aliaga dunia siku ya Jumamaosi akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa takriban miaka minane.
Atazikwa baadaye leo katika shamba la familia yake jangwani Negev.
Maelfu ya waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho kwa Sharon siku ya Jumapili wakati ambapo mwili wake ulikuwa umelazwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem.
Na TheChoice
Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon afariki Dunia.

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon afariki Dunia.



Picha ya waziri mkuu wa zamani Ariel SharonPicha ya waziri mkuu wa zamani Ariel Sharo
Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon, amefariki dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 85.

Alikuwa waziri mkuu wa Israel mwaka 2001.Amekuwa mahututi tangu mwaka 2006 kufuatia mfululizo wa matatizo ya kiharusi. Ariel Sharon alikuwa askari wa vita na baadae kuwa kiongozi wa nchi.

Alipokuwa mwanajeshi, alijulikana kwa ushujaa wake katika uwanja wa mapambano kwa miongo kadhaa kufuatia kuundwa kwa taifa la Israel, akijulikana hasa wakati wa vita vya jom kippur vya mwaka 1973. Katika mbinu za hali ya juu alizozionyesha, aliwaongoza wanajeshi wa Israel kuvuka mfereji wa suez, na kulikabili jeshi la misri.

Pia alijulikana na wengi kwa kuwa jabari na mbabe. Mwaka 1982, aliongoza uvamizi wa Lebanon ambao ulipelekea mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wa Lebanon kwa mamia ya wapalestina katika kambi za wakimbizi za sabra na shatilla huko Beirut.

Kama mwanasiasa, Ariel Sharon pia alikuwa na utatanishi. Akiwa waziri, alihamasisha kuundwa kwa makazi ya walowezi wa kiyahudi kote katika maeneo ya wapalestina.

Serikali yake ilizikandamiza vurugu katika muda wa miaka michache, na kuanza kazi ya kuweka vizuizi vya usalama ambavyo hivi sasa vinawatenga waisraeli na wapalestina.

Mwaka 2006, bwana Sharon alipata mfululizo wa matatizo ya kiharusi na kuingia katika hali ya kupoteza fahamu. Nafasi yake ya waziri mkuu ilichukuliwa na Ehud Olmert.
na Voaswahili

Kategori

Kategori