Mapigano yapamba moto mjini Malakal, Sudan Kusini

Jeshi la Sudan Kusini limepambana leo na jeshi la waasi katika mji mmoja muhimu wakati majeshi yakiwafurusha waasi katika mji mwingine, baada ya kuukomboa.
Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa ukiidhinisha kuongezwa maradufu idadi ya wanajeshi wake wa kulinda amani nchini humo. Maelfu wanaaminika kuuwawa katika kipindi cha zaidi ya wiki moja iliyopita, wakati kukiwa na ripoti za miili kupatikana katika makaburi matatu ya pamoja. 

Majeshi ya serikali yamesheherekea jana baada ya kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa wanajeshi wanaomuunga mkono makamu wa rais Riek Machar, lakini makabiliano yameendelea kwingineko ikiwa ni pamoja na Malakal, mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile.
Na Dw.deswahili