VYUO vinavyo toa elimu mbalimbali hapa nchini vimekuwa vikikosa wanafunzi kwa wakati kutokana na kuwapo kwa utandawazi.
Akizungumza katika maafari ya kuhitimu wanachuo wa katika ngazi ya cheti na Diploma ya uandishi wa habari mkoani Mbeya Mkurugenzi wa chuo cha uandishi wa habari cha Royal cha Mbeya Uswege Kagubo alisema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kuwapata wanafuzi kutokana na utandawazi.
Alisema Chuo kilianzishwa ili kuwakombo wananchi wa mbeya ambao walishindwa kuendelea na kidato cha tano lakini wamekuwa hawajitokezi kujiendeleza kielimu na kuwa wanataaluma.
Nae mgeni rasmi katika maafari hayo, Japheth Mwasandube, ambaye ni mhadhili mstaafu katika chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku) aliwaka wahitimu hao baada ya kumaliza elimu zao wasiwe waoga katika uandishi wao ambapo waandike ukweli bila kujali maslahi ya mtu am baye anapinga ukweli.
Alisema waandishi wanafulsa ya kuingia kila mahali na kuandika habari na kuwahabarisha ambao hawawezi kuingia kila mahali.
“Alisema kuwa waandishi wa habari mnaweza kuwahabarisha wananchi mambo ambayo wao walikuwa hawayajui na kukaa katika majeshi na kuwajulisha wananchi ambao hawawezi kuingia katika maeneo kama hayo ambako kuna vita” alisema Mwasandube.
Aliongeza kuwa kufuatia kuwapo kwa umuhimu wao huo waandishi hao wakiingia mtaani wasiwe waoga kufanya kazi yao ambayo ni muhimu kwa jamii.
Mwasandube alisikitishwa na kuwapo kwa uonevu wa waandishi wa habari ambapo wamekuwa ni watu muhimu kwa kupewa nafasi ndogo katika jamii na hivyo kuwataka wakajipiganie kuhakikisha wanapewa nafasi yajuu serikalini hasa katika kutetewa na serikali katika maslahi yao.
Kwa upande wake mmjoja wa waalikwa kjatika maafali hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mbeya, Ulimboka Mwakilili alisema kuwa ili kupambana na soko la ajila hapa nchini wanachuo hao wajitume kusoma katika kozi mbalimbali ambazo zitawasaidia kuajiliwa mapema.
Mmjoja wa wahitimu katika chuo hicho na alikuwa wa pekee katika ngazi ya Diploma, Stephano Simbeye, alisema kuwa waandishi wa habari wasilizike na elimu walizo nazo kwa kuto wenda kujiendeleza.
Alisema wanahabari ni vema wakajiendeleza katika elimu zao ili kufanya kazi zao kwa weledi na kuhakikisha elimu yao inakuwa ya juu kuliko kubaki na elemu zao zilezile walizo anzanazo kazi hata miaka kumi bila kwenda shule.
“Nataka kutoa wito kwa wanahabari wenzangu kuto bweteka na elimu walizonazo wajitahidi kwenda kujiendeleza mara kwa mara ili kuongeza ufanisi katika elimu zao waandishi msilizike na elimu zenu hizo,” alisema Simbeye.