DIWANI wa kata ya Ngonga wilayani Kyela ameilamikia
serikali juu ya tatizo la kutokuwepo kwa utatuzi wa tatizo la maji linaloikabili kata hiyo kwa kipindi kirefu tangu nchi kupata uhuru mpaka mwaka 1961.
Kauli hiyo ilisemwa na diwani wa kata hiyo Kileo Kamomonga, jana ofisini kwake akiwa na waandishi alisema, kuwa kumekuwa na tatizo la maji kwa kata yake kwa muda mrefu na kuwa wananchi wamekuwa wakikosa huduma ya maji safi na salama.
Kamomonga aliongeza kuwa aliomba kutengewa fedha na serikali kwa ajili ya ujenzi wa kisima kilichopo Ndongwa lakini fedha hazijaingia toka kwenye mfuko wa Benki ya dunia hivyo kushindwa kukamilisha mradi huo.
Alisema kuwa kuna kisima kilicho chimbwa cha maji ambacho kinatoa maji machafu yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu kwa kile alichodai kuwa yana vumbi ambalo inafanya kisima kisitumiwe maji na huku kuna uhitaji
wa maji kwa wananchi.

“Kisima kimoja kilichimbwa eneo hili ambapo mbunge alisema kuwa atakuja kutuwekea visima vingine hadi sasa imekuwa ni ahadi na niliomba fedha serikalini kwa ajili ya mradi wa maji lakini sikupewa fedha hizo ambapo wananchi wangu wamekuwa na tatizo hili la maji kwa muda mrefu” alisema Kamomonga.
Diwani huyo alisema kuwa kuna uhitaji wa pampu maalumu kwa ajili kuweza kuvuta maji toka chini ya kisima hadi kupeleka kwenye tanki ambalo litakuwa likitwamisha maji na uchafu unaweza kupungua.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi hao Edward Ngusa alisema wameshindwa kutoa hamasa kwa wananchi wake katika shughuli zingine za kimaendeleo kwa kuwa kuna baadhi ya kazi za maendeleo zinazotakiwa kufanywa kwa kutumia maji.
Ngusa alisema kuwa imefikamwafaka wa kuwa serikali itekeleze ahadi zilizo kuwa zimeahidiwa kwa wananchi ili kuweza kufanikisha utendaji wa kazi za kimaendeleo na kuwa na imani na serikali kuliko kuahidikila matekelezo.
Alisema kuwa mradi huo wa kisima ukitekelezwa utakuwa na manufaa hata kwa vijiji vingine ambavyo ni Katumba Songwe na Mpuguso ambapo nako kuna tatizo la maji kwa muda mrefu na kutasaidia kuokoa maisha ya wananchi kwa kuwa wataanza kutumia maji safi na salama kwa afya yao.
Mkazi huyo alitoa lawama kwa mbunge wa wilaya hiyo kuwa ahadi zake zimeshindwa kukamilika nawakati muda wake unazidi kuisha bila kuona mafanikio ya maji kwa wananchi wa kata hiyo ya Ngonga.

Na Mwandishi wetu Kyela