WATU watatu wamefariki dunia baada ya magari mawili kuvaana Uso kwa uso katika ajali iliyo tokea naeneo ya Mashara Kata ya Igurusi wilayani Mbearali mkoani Mbeya na kujeruhi akiwembo mganga mtafiti.
Katika ajali hiyo iliyo husisha roli lenye namba za usajili T.843 CKL na tera namba T693 CKL ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Mugoni Lusenga liligongana uso kwa uso na Toyota saloon yenye namba za usajili T.830 BQJ.
Toyota hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Mganga mtafiti Godfrey Bonifas ambaye alijeruhiwa na kula za katika hospitali ya Chumala wilayani Mbarali.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Barakael Masaki alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Disemba 24 mwaka huu
na kusababisha vifo vya watu watatu ambao hata majina yao hayajafahamika.
Alisema watu hao walio kufa walikuwa katika Toyota Saloon na kuwa kati yao wanawake walikuwa wawili na mwanaume mmoja.
Alisema kuwa wananchi wawe makini watumiapo vyombo vya moto barabarani hasa kipindi hiki cha sikukuu.
Akisimulia tukio hilo Masaki amesema kuwa Toyota ilikuwa ikitaka kuipita gali yenye namba za usajili T.843 CKL/T.693 CKL na dereva wa kali hiyo anashililiwa.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dreva aliyekuwa akiendesha Toyota Saloon.