WAALIMU NDANI KWA KUIBA MITIHANI

MAHAKAMA ya wliya ya Rungwe mkoani Mbeya imewahukumu kwenda jela miaka nane walimu wawili
kwa kosa la kuiba mtihni wa darasa la saba huku wanafunzi
watatu ikiamuru kuchapwa viboka 13, ambao waliofanya njama za kuibamtihani wa maarifa ya jamii.

Mwendesha mashitaka John Kyejo akisoma maelezo ya kesi alisema kuwa watuhumiwa watatu  ambaoni wanafunzi waliofanya njama za kuiba mtihani huo kuwa ni Kosintatin Agustino ambaye kwa sasa ana miaka (21), Aswile Kapunga ambaya ana miaka (18), na Aswile Mwakasekele ambay kwa sasa ana miaka (20) walio kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ibungu.

Alisema kuwa kuwa watuhumiwa hao walifanya koso hilo la kuiba mtihani Septemba kumi mwaka 2009 ambapo waliiba mtihani wa maarifa ya jamii na kuweza kuupeleka kwa walimu kwa ajili ya kufanya ilikupewa majibu ya mtihani huo.

Kyejo alisema watuhumiwa hao walikabiliwa na makosa matatu ambapo waliwasilisha nyalaka zilizoifadhiwa ambapo ni kinyume na sheri ya kifungu namba nne kidogo cha B kwa ajili ya watoto na kuwa kosa la pili lilikuwa ni walimu kupokea nyalaka hizo kinyume na saheria ya nne kifungu kidogo cha tatu.

Aliendela kueleza kuwa kosa la tatu lilikuwa ni kula njama kinyume na fungu 384 ya sheria ya adhabu juzu ya 16 ya mwaka 2002 ambapo tarehe nane na kumi watuhumiwa wote hao walikula njama ya kuiba nyaraka hizo za kuvujisha mtihani huo wa maarifa ya jamii.

Akitoa adhabu hiyo hakimu mkazi mwandamizi Omary Kingwele alisema kuwa watuhumiwa watatu ambao walikuwa ni wanafunzi watachapwa jumla ya viboko 13 na kuachiwa kwa ajili ya kuweza kuelimisha jamii kluondokana na tabia mbaya kaza hizo ambazo zina madhara.

Kingwele alisema kuwa katika kosa la pili walimu hao walifanya ni
kupokea taarifa hizo knyume na kifungu cha sheria ya nne kidogo cha tatu ambapo walimu hao waliadhibiwa kufungwa kifungo cha miaka sita jela.

Aliongeza kuwa katika kosa la tatu watuhumiwa hao wamehukumiwa kufungwa miaka miwili kwa kosa la kula njama na kinyume na fungu 384 ya sheria adhabu ya juza 16 ya mwaka 2002 na kuwa adhabu hizo zitaenda
kwa pamoja.

Na Mwandishi wetu Rungwe