Tanzania yahuzunishwa na tabia ya nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya, Uganda na Rwanda, ambazo
ziliamua kuiweka pembeni Tanzania na kuunda "umoja wa nia", Rais Jakaya
Kikwete aliliambia bunge Alhamisi (tarehe 7
Novemba7).
Kikwete aliwaambia watunga sheria katika hotuba ya kitaifa
iliyotangwazwa na televisheni kwamba nchi wanachama tatu zimejitenga
zenyewe na kujiendesha kinyume na Mkataba wa EAC na itifaki ya1999,
jambo ambalo halikubaliki.
"Wameunda umoja wa nia, nani asiye na nia?" Kikwete alisema.
Kenya, Uganda na Rwanda zilikutana mwezi uliopita huko Kigali, pasipo wanachama wenzao wa EAC Tanzania na Burundi.
Watatu hao waliazimia kuhusu masula manane, lakini Tanzania inahusika
zaidi na jitihada zake za kuunda kamati iliyopewa kazi ya kuandika
katiba ya EAC na uamauzi wao wa kuunda umoja wa forodha, "ambao ulipaswa
kujumuisha wanachama wote wa jumuiya", Kikwete alisema.
Tanzania inachangia shilingi bilioni 12 (dola bilioni 1.3) kwa mwaka
kuendesha masuala ya EAC, kwa hiyo ni makosa kusema Tanzania haikutaka
kuharakisha mchakato wa muungano wa EAC, raisi alisema.
Alisema nchi hizo tatu zinataka kujiwahisha kwenye hatua inayofuatia
ya kuunda shirikisho kabla ya kukamilisha hatua tatu za mwanzo
zinazotakiwa kisheria na mkataba na itifaki. .
"Mkataba uko wazi. Unatuwekeza kuanza na umoja wa forodha, soko la
pamoja, fedha moja na baada ya hapo shirikisho," Kikwete alisema.
"Tunataka kujenga msingi imara wa uchumi ambao utatoa uhakikisho wa
shirikisho."
Alisema nchi wanachama wote wa EAC zilikutana Arusha
tarehe 28 Aprili na kukubaliana kutoa ripoti kwenye mkutano wa wakuu wa
nchi uliopangwa kufanyika tarehe 30 Novemba huko Kampala. Lakini mwezi
Juni, nchi hizo tatu ziliamua kujitenga, pasipo kushirikisha Tanzania.
Hahari na Sabahi Online
Subscribe to:
Post Comments (Atom)