MZOZO WA KIKATIBA MALDIVES

Mahakama Kuu nchini Maldives imeamuru kusitishwa kwa marudio ya uchaguzi wa urais yaliokuwa yafanyike leo hii.


Mahakama hiyo imesema tarehe muafaka ya kufanyika kwa marudio hayo ya uchaguzi itakuwa Novemba 16. Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Maldives, Mohamed Nasheed alipata ushindi wa asilimia 47 ya kura za wananchi katika uchaguzi uliofanyika hapo jana wakati Yaamin Abdul Gayoom kaka wa kiongozi wa zamani wa kiimla nchini humo alifuatia kwa kujipatia asilimia 30 ya kura.

Marudio ya uchaguzi inabidi yaendelee kufanyika hadi pale mgombea atakapojipatia angalau asilimia 50 ya kura.

Uamuzi huo wa mahakama kuu unaweka uwezekano wa kuzuka kwa mzozo wa kikatiba ambao utawatenga na kuwagawa wapiga kura na kuiweka hatarini demokrasia changa ya nchi hiyo.