Ghasia zazuka upya mjini Tripoli

Mapigano yamezuka upya mjini Tripoli hii leo, wakati idadi ya vifo vilivyotokana na maandamanao ya kupinga makundi ya waasi katika mji huo mkuu wa Libya ikiongezeka hadi 40. 
Zaidi ya watu 400 pia wamejeruhiwa wakati maandamano hayo ya jana yalipogeuka kuwa vurugu na kuendelea usiku kucha. Waziri wa Sheria Salah al-Marghani amesema idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka. 
Mapigano mapya yamezuka wakati magari yaliyojaa waasi wa Misrata wakielekea katika mji mkuu Tripoli wakitokea katika viunga vya mashariki vya Tajura. 
Waziri Mkuu Ali Zeidan ametoa wito wa "kuvumiliana na kusitisha ghasia" huku akionya kuwa kuwepo magari zaidi ya kivita katika mji huo mkuu "kutafanya hali kuwa mbaya zaidi". 
Waziri Mkuu Ali Zeidan amekuwa
akijitahidi kudhibiti wanamgambo, waasi walio na itikadi kali za kidini na waasi wa zamani waliokataa kusalimisha silaha zao miaka miwili baada ya kuondolewa na kuuwawa kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddaffi. 
Na Dw.de 

Related Posts