Showing posts with label June 09. Show all posts
Showing posts with label June 09. Show all posts
PICHA: KOREA KASKAZINI YAANZISHA MAFUNZO YA KIJESHI KWA WATOTO WADOGO

PICHA: KOREA KASKAZINI YAANZISHA MAFUNZO YA KIJESHI KWA WATOTO WADOGO

Korea Kaskazini yaanzisha mafunzo ya Kijeshi kwa watoto nchini humo kuwaandaa na mapambano dhidi ya “ukoloni wa Marekani” na kumlinda Rais wao mpendwa, Kim Jong-un.
Mwalimu katika shule hiyo ya Kijeshi amesema, “Watoto wetu wanajua kuwa Rais Kim Sung wa pili na jenerali Kim Jong wa pili ni baba zao na katika shule hii wanajifunza kwa bidii kama wanavyotaka. Hiki ni Chuo cha hali ya juu kabisa kinachoandaa Jeshi la Korea.”
“Tunasoma kwa bidii kwa sababu tunajua hivyo ndio tutakavyoweka kulipa kisasi dhidi ya ukoloni wa Marekani. Ninasoma kwa bidii nipate ufaulu wa juu kwenye masomo ya Kijeshi kama vile mbinu za kivita na kulenga shabaha,” ni kauli ya mmoja ya wanafunzi vijana katika chuo hicho.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rILwtD
via IFTTT


TUNDU LISSU: NITAKATAA NAFASI YOYOTE NITAKAYOTEULIWA NA RAIS MAGUFULI

TUNDU LISSU: NITAKATAA NAFASI YOYOTE NITAKAYOTEULIWA NA RAIS MAGUFULI

Swali: Tumeona kuwa sasa hivi Rais anachukua watu kutoka upinzani na kuwapa nafasi katika serikali yake, unalichukuliaje hili?
Lissu: Hao sio wapinzani na hawajawahi kuwa wapinzani, walianzishwa kwa ajili ya kuua upinzani – imeshindikana na sasa wanazawadiwa. ACT na Anna Mghwira walikuwa wakabiliane na Lowassa, sio wakabiliane na CCM, walipata kura elfu tisini na ngapi sijui hawakufika hata kura laki moja. Sasa, huu ukuu wa mkoa ni zawadi tu. Ukatibu mkuu wa Kitila Mkumbo ni kuwazawadia watu wao. Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haijawahi kuwa na shida na ACT, haijawahi kuwa na shida na Anna Mghwira, haijawahi kuwa na shida na Kitila Mkumbo na haijawahi kuwa na shida na ‘hao wote wanaojiita wapinzani.’ Shida yao kubwa ni CHADEMA, shida yao kubwa ni CUF. Hao ndio wapinzani, wengine wote hawa ni wana CCM. Wengine wamevaa gwanda hili, wengine wamevaa gwanda lile. Wote ni wana CCM kwa sababu wanafanya kazi za CCM.
Swali: Labda itokee Mh. Rais amekuteua kwenye nafasi yoyote ile ambayo ana mamlaka nayo, itakuwaje?
Lissu: Kwanza haitatokea, nikutoe wasiwasi. Pili, hata ikitokea Rais akafanya hivyo, nitamwambia mheshimiwa mimi napinga mfumo uliokuweka madarakani. Tunataka Katiba mpya, tunataka tutengeneze nchi upya. Kwahiyo kwanza hawezi na pili akinijaribu nitamwambia wazi kwamba kama unataka niitumikie nchi hii tubadilishe Katiba na tuiweke nchi sawa kwenye misingi sawa. Lakini mimi siwezi kutumikia utawala wa kidikteta kwa nafasi yoyote ile. Mimi ni mpinzani, na ndio maana nipo Mahakamani kila siku. Wanaopewa hizo nafasi sio wapinzani, ni watu wanaotumiwa kuua upinzani na hawataweza.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rU95Oq
via IFTTT


RAIS KIKWETE AELEZA CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO KWENYE KULIMA MANANASI

RAIS KIKWETE AELEZA CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO KWENYE KULIMA MANANASI

. Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.
Akizungumza leo Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.
“Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu,” amesema.
Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.
“Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,”amesema.
Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.
Mwananchi

from Blogger http://ift.tt/2rIEp4i
via IFTTT


Exclusive. Hatimaye Nabii Frank Afichua Kiini cha Mauaji ya Kibiti na Rufiji..!!!

Exclusive. Hatimaye Nabii Frank Afichua Kiini cha Mauaji ya Kibiti na Rufiji..!!!

Akizungumza mapema asubuhi ya leo na Kituo cha Luninga cha Channel Ten na Magic fm Radio Nabii anayekuja kwa Kasi nchini Nabii Frank leo amefunguka na kueleza mambo makuu mawili ambayo ndiyo chanzo cha mauaji yanayoendelea Kibiti na Rufiji na amezitaka Mamlaka husika kuyafanyia Kazi ili kumaliza mauaji.
Amesema kwamba mauaji hayo yanatokana na sababu za Harakati za Kidini ( yaani kuna dini moja inataka kuwa ndiyo inayoaminika na kukubalika katika huo Ukanda hivyo wanaua Watu hasa wa dini fulani ili kuwatisha na wakimbie au wahame hayo maeneo na wabaki wao tu ) na sababu ya pili kasema kwamba Mfumo wa Kiuchumi wa Watu wa hayo maeneo umeharibiwa hivyo Wauwaji wameamua sasa kuwauwa wale wote ambao wanahisi ndiyo chanzo cha Mfumo wao huu kuharibiwa. Na inasemekana kwamba Mfumo mkubwa wa Kiuchumi au uingizaji Kipato kwa asiimia kubwa ya Watu wa hayo maeneo ni Mkaa na kama tunavyojua Serikali imepiga marufuku huku ikiweka Sheria kali dhidi ya wale watakaokamatwa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sKFMh8
via IFTTT


Hivi ndivyo majibizano kati ya Costa na Conte yalipoanzia.

Hivi ndivyo majibizano kati ya Costa na Conte yalipoanzia.

Baada ya msimu kumalizika kocha wa Chelsea Antonio Conte aliamua kuongea na wachezaji wake kupitia ujumbe mfupi wa message ambapo aliwapongeza kuhusu msimu uliopita na kuwaambia matarajio yake juu yao kuhusu msimu ujao wa ligi kuu ya Epl.
Chanzo kimoja cha habari kimedai Antonio Conte hakumtumia Costa message mbaya lakini alimuambia maoni yake kama kocha lakini Mhispania huyo hakupendezwa na maoni ya Conte hivyo akamjibu Conte vibaya na ndipo Muitaliano huyo alipokasirika na kumuambia Costa kuwa hamtaki katika kikosi chake.
Costa kuona amejibiwa vibaya na Conte naye akaanza kumjibu vibaya hali iliyopelekea wawili hao kutumiana message mbovu na baadae Diego Costa alikasirika sana akaamua kutuma message hizo kwa wachezaji wote wa Chelsea aliokuwa na namba zao.
Tayari mgogoro huo umechukua sura mpya kwani mmiliki wa klabu ya Chelsea tajiri Roman Abromovich amechagua upande wake katika pande hizo mbili zinazovutana na Roman anaona hakuna mchezaji mkubwa kuliko kocha hivyo na yeye yuko upande wa kocha wao.
Chelsea wanapambana kutafuta mshambuliaji namba 9 ambaye anaweza kuziba nafasi ya Diego Costa na ugomvi kati ya Costa na Conte umezidi kuisukuma Chelsea kutafuta saini ya mchezaji wao wa zamani Romelu Lukaku ambaye thamani yake inatajwa kuwa euro 100m.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2smd2OF
via IFTTT


Hii ndio klabu inayoongoza kwa idadi kubwa ya makombe Ulaya.

Hii ndio klabu inayoongoza kwa idadi kubwa ya makombe Ulaya.

5.Juventus. Msimu huu walionekana bora sana na walitabiriwa na wengi kwamba huenda wangeweza kuchukua ubingwa wa Champions League lakini wakafungwa na Real Madrid. Juventus ndio klabu inayoongoza kwa mafanikio nchini Italia kwani wameshashinda Serie A mara 33 wakashinda Italian Cup mara 12 na Italia Super Cup mara 7,Champions League mara 2,Europa League mara 3 na kombe la washindi mara moja,Uefa super cup mara mbili,klabu bingwa dunia mara mbili na kuwafanya jumla kuwa na makombe 62.
4.Manchester United. Hii ndio klabu inayoongoza kwa mafanikio nchini Uingereza ikiwa imeshashinda vikombe 20 vya ligi kuu nchini Uingereza huku wakiwa wamebeba Fa mara mara 12, vikombe vya ligi mara 5 na mara 21 wakibeba ngao ya hisani,kombe la washindi mara moja,super cup mara 1,intercontinental cup mara 1,klabu bingwa dunia 1 na makombe makubwa ya Ulaya wameshashinda mara 4 huku mwaka huu wakibeba kombe la Europa ambalo walikuwa hawajalibeba kwa siku nyingi na jumla pamoja na makombe ya vilabu vya dunia na mabara United wameshinda vikombe 66.
3.Bayern Munich.Wana vikombe vya Bundesliga mara 27 huku wakiwa na vikombe vya ligi ya Ujerumani mara mara 6,German Cup mara 18, German Super Cup mara 5, nje ya Ujerumani klabu hii imeshashinda makombe ya Ulaya mara 5,Intercontinental cup mara 2 huku wakiwa wameshinda kombe klabu bingwa dunia mara moja, kiujumla klabu hiyo ya Ujerumani imechukua jumla ya makombe 67 hadi sasa.
2.Real Madrid. Wamefanikiwa kutetea kombe la Champions League na hiyo ikawapa kombe hilo kwa mara ya 12 ya makombe ya ya Uefa, Uefa super cup mara 3,klabu bingwa dunia mara 2, La Liga mara 33, Copa Del Rey mara 19, 9 Spanish super cup,intercontinental cup mara 3,Spanish League Cup 1 na Europa 2 hii ikiwapa jumla ya makombe 84.
1.Kama mpira ni makombe baasi Barcelona ndio klabu bora barani Ulaya kwa sasa kwani ndio klabu inayoongoza kuchukua makombe mengi ulimwenguni kuliko klabu nyingine yoyote, wameshashinda ubingwa wa La Liga mara 24,Spanish Cup 29,Spanish Super Cup mara 12,Spanish League Cup mara 2,klabu bingwa dunia mara 3, na mwaka 2009 walishinda makombe 6,makombe 5 ya Ulaya,kombe la washindi mara 4,Uefa super cup mara 5 lakini jumla Barcelona wana makombe 87.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sbf04x
via IFTTT


Kategori

Kategori