WAKAZI wa mtaa wa
Idundundilanga maeneo ya Chaugingi halmashauri ya Mji na Mkoa wa Njombe Nyanda
za juu kusini mwa Tanzania wameishutumu serikali kupitia darali ambaye anaondoa
vibanda vya wafanyabiashara wadogo pembezoni mwa barabara za mji huo kwa kuto
toa elimu kwa wafanyabiashara juu ya zoezi hilo la uvunjaji wa vibanda na meza
za biashara.
Wakizingunza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa zoezi hilo
limekuwa ghafla kwa kuwa awali wakipatiwa taarifa za uondoa vibanda vyao
hawakuambiawa waondoe meza pekee na wengine wakisema hawakuambiwa muda wa
kuondoa vibanda vyao.
Aidha baadhi ya wakazi wa mtaa huo ndio walikuwa wanategemea
kununua mboga mboga katika mitaa hiyo wanasema kuwa soko linakotakiwa kuwepo ni
mbali sana na makazi yao bora kama kila mta ungekuwa na soko ili huduma za
mahitaji wazipate hapo.
Kiongozi wa zoezi hilo ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya
udalali ya Igagara Kawe Msango anasema kuwa Mji utakuwa safi kwa kufanywa na
wakazi wenyewe na haiwezekani mji ukasafishwa na wageni ndio maana wapo kazini
kufanya kazi hiyo ili kuweka mji safi kwa niaba ya mkurugenzi.
Katika zoezi hilo Mgamo walio chini ya kampuni hiyo
wamefanya shuguri zao wakiwa na mashoka kwaajili ya kuangusha mabanda yoto na
kuvunja meza zilizo sehemu isiyo rasimi.
READ MORE.........
Bonyeza hapa kwa Video zaidi ==> VIDEOZ