ASKARI wa jeshi la wananchi kikosi cha 514 KJ Makambako Mkoani
Njombe ameuwawa kwa kupigwa Risasi na askali wa jeshi la polisi ambao walikuwa
ni wachumba baada ya kutokea kwa ugomvi baina yao.
Askari wa jeshi la Polisi H 2299 Zakaria Dotto (25) amempiga
risasi mbili askali wa jeshi la Wananchi Neema Masanja (25) Mkazi wa Mtaa wa
Jeshini kata ya Maguvani mjini Makambako mkoani Njombe Njanda za juu kusini mwa
Tanzania ambaye wakitarajiwa kuwa mke majira ya saa 12 asubuhi.