Ramadhan Singano apata ofa nne mpya, Yanga nao wamo

KIUNGO wa Azam Fc Ramadhan Singano ‘Messi’ Baada ya kugoma kusaini mkataba mpya Azam sasa amepokea Ofa nne mezani kwake kutoka klabu za Tanzania.
Messi ambaye mkataba wake unamalizika Julai 8 mwaka huu ameamua kuangalia maisha sehemu nyingine na kuachana na Azam kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo maslahi.
Shaffiidauda.co.tz.ilizungumza kaka wa Ramadhan Singano amedhibitisha mdogo wake kupokea ofa nne kutoka Tanzania ikiwemo ya klabu ya Yanga.
“Ni kweli dogo amepokea ofa kutoka vilabu vinne vya Tanzania (Yanga, Singida United, Stand United na Lipuli Fc) Tunasubili mkataba wake uishe ili tuangalie ofa nzuri “alisema Kaka yake Singano
Singano na Azam wameshidwa kuelewana kwenye kuongeza mkataba mpya baada ya Azam kumpa ofa ya milioni kumi na mshahara wa 1,150,000 kwa mwezi.
Wakati yeye Singano akiwaomba wampe milioni 20 na mshahara wake uendelee kubaki millioni mbili Kwa mwezi kama anavyolipwa sasa hivi na kama hilo wameshindwa ni bora aondoke.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rUIQLb
via IFTTT