Dani Alves aruhusiwa kuondoka Juventus.

Ni msimu mmoja tu umepita tangu Dani Alves ajiunge na klabu ya Juventus akitokea katika klabu ya Barcelona lakini sasa Dani Alves ameruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo.
Mkurugenzi wa klabu ya Juventus bwana Giussepe Marotta amethibitisha kwamba mlinzi huyo raia wa Brazil hatakuwepo katika klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi.
Marotta amekiri kwamba klabu yao bado ilikuwa ikimhitaji Alves lakini hawawezi kuwa naye wakati yeye mwenyewe kama mchezaji hataki kubaki katika klabu hiyo.
“Tunamtakia kila la kheri huko anakokwenda na alikuwa mtu mzuri sana kwetu lakini hatutakuwa naye katika msimu ujao wa ligi” alisema Marotta.
Habari hii inaweza kuwa njema kwa mashabiki wa Man City kwani Dani Alves amekuwa akiwindwa na kocha Pep Gurdiola na taarifa hii inaweza kuonesha kwamba yuko njiani kuelekea Etihad.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sTqCsy
via IFTTT