“VAR ingekuwepo 2006 tungebeba UEFA” Arsene Wenger.

Teknolojia ya Video Assistant Referee(VAR) imeanza kutumiaka rasmi katika baadhi ya ligi barani Ulaya na huku ikiungwa mkono na watu wengi lakini wengine wachache wakiiponda teknlojia hiyo kwa kudai inapunguza utamu wa soka.
VAR yenyewe inakuwa inamsaidia muamuzi kufanya maamuzi uwanjani kwa kuangalia Video za tukio lililofanyika ambapo itamsaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na tukio husika.
Kocha Arsene Wenger naye ameibuka kuzungumzia VAR ambapo amesema teknolojia hiyo imechelewa kuja na kuchelewa kwa ujio wa teknolojia hiyo kumeifanya Arsenal kukosa ubingwa wa michuano ya UEFA mwaka 2006.
“Mwaka 2006 tulikuwa tunaongoza kwa bao 1 kwa sifuri zikiwa zimebaki dakika 30 kwa mchezo kuisha, lakini Barcelona wakapata bao ambalo lilikuwa la offside” alisema mzee Wenger.
Wenger anaamini kama teknolojia ya VAR ingekuwepo baasi wangeweza kumaliza mchezo huo huku wakiongoza kwa bao hilo moja na kutwaa ubingwa huo ambao hajawahi kuunyanyua.
Wenger pia anasema kila akilikumbuka bao la Roberto Lewandoski dhidi yao huwa wazo la teknolojia hiyo ta video inamjia akilini sana na sasa anaona ni bora tu ianze kutumika ili kuiokoa timu yao na majanga ya mabao ya offside.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rUkgK6
via IFTTT