Timu ya taifa ya Ureno ilikuwa uwanja wa ugenini kuikabiri timu ya taifa ya Latvia ambapo Ureno waliibuka kidedea kwa mabao matatu kwa sifuri huku mabao ya Ureno yakiwekwa kimiani na Cristiano Ronaldo aliyefunga mara mbili na Andre Silva akifunga moja.
Mabao hayo ya Cristiano Ronaldo yamemfanya afikishe jumla ya mabao 73 ambapo anakuwa mchezaji wa 3 kuwahi kuifungia timu yake ya taifa mabao mengi zaidi katika bara la Ulaya, katika mchezo mwingine timu ya taifa ya Uholanzi imeshusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Lexembourg cha mabao matano kwa sifuri.
Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Arjen Robbben,Wesley Sneijder,Wijnaldum,Quincy Prommes na Vincent Jenssen waliofunga moja moja huku Belarus wakiifunga Bulgaria kwa mabao mawili kwa moja, Andorra wakaifunga Hungary bao moja kwa sifuri,
Ubelgiji kupitia kwa Mertenes na Nacer Chadli waliifunga Estonia mabao mawili kwa sifuri na Switzerland nao wakaifunga Faroe mabao mawili kwa nunge, Ugiriki na Bosnia wakatoka uwanjani bila kufungana huku Cyprus wakiifunga Gibraitar mabaop mawili kwa moja.
Timu ya taifa ya Sweden ilikuwa nyumbani kuikabili Ufaransa na wakafanikiwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuibwagiza Ufaransa mabao mawili kwa moja na mabao ya Sweden yakifungwa na Jimmy Durmaz na Ola Toivonen huku lile la Ufaransa likifungwa na Olivier Giroud.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2t5seME
via IFTTT