Showing posts with label June 10. Show all posts
Showing posts with label June 10. Show all posts
VYAKULA VINAVYOONGEZA KUVU ZA KIUME

VYAKULA VINAVYOONGEZA KUVU ZA KIUME

Moja ya biashara ambayo imeshamiri katikati ya miji hasa Dar es salaam ni biashara ya mihogo mibichi, nazi na karanga mbichi. Kwa utafiti mdogo kwa njia ya kuuliza watumiaji na wauzaji wanasema kuwa vyakula hivyo vinaongeza mbegu za kiume.
Leo nitawaletea maelezo ya kitaalamu ni aina gani ya vyakula ambavyo husaidia kuongeza idadi ya mbegu za kiume zenye afya na ujazo wake na faida zingine za afya ya uzazi.
Mayai ni moja ya vyakula vinavyokubalika kitaalamu kusaidia kuongeza wingi wa mbegu za kiume na vile vile kusaidia kuongeza kasi ya mbegu za kiume kutokana na mayai kusheni vitamin E na protini, ambayo vyote kwa pamoja husaidia kulinda mwili kutokana na sumu za radiko ambazo hupunguza wingi wa mbegu za kiume.
Vilevile virutubisho hivyo vilivyopo katika yai husaidia kutengenezwa kwa mbegu imara zenye afya jambo ambalo ni muhimu kwa urutubishaji wa kijiyai cha kike.
Spinachi ni moja ya mbogamboga ambayo inakubalika kusheheni tindikali ya foliki ambayo ni muhimu sana katika utengenezwaji wa mbegu za kiume, ingawa mboga zote za kijani zinakubalika kutokana na kusheheni vitamini mbalimbali.
Pale mwanaume anapokuwa na kiwango kidogo cha foliki, husababisha kuzalisha mbegu za kiume zisizo timilifu. Mbegu za namna hii zinakuwa na wakati mgumu katika kufikia na kupenya katika tando za kijiyai cha kike wakati wa urutubishaji. Hali kama hii inaweza kusababisha kuzaliwa mtoto mwenye hitilafu za kimaumbile kwa sababu ya kijiyai cha kike kurutubishwa na mbegu zenye hitilafu.
Ndizi ni moja ya tunda ambalo limesheheni vitamin A, B1, na C ambazo husaidia mwili kutengeneza mbegu za kiume zenye afya na vile vile kuongeza wingi wa mbegu hizo. Pia, ndizi huwa na kimeng’enya adimu kijulikanacho kitabibu kama Bromelain ambacho huzuia milipuko wa kinga ya mwili, hivyo husaidia kuongezeka wingi wa mbegu za kiume pamoja na kasi yake.
Chokoleti yenye rangi ya kahawia iliyokolea inajulikana zaidi duniani na ndiyo maana katika hoteli kubwa huweka ndani ya vyumba vya wanandoa waliopo fungate. Sababu kubwa ni kutokana na aina hii ya chokoleti kuwa na tindikali ya amino (protini) ijulikanayo kama L-Arginine HCL ambayo husaidia kuongeza ujazo wa mbegu za kiume na wingi wake. Vilevile huongeza msisimko wa kilele cha tendo la ndoa.
Mboga ijulikanayo kama Asparagus ambayo huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C ambayo ina wigo mkubwa katika kusaidia utengenezwaji wa mbegu za kiume. Vitamin C hutoa ulinzi kwa seli zilizopo katika kokwa za kiume (kende) zisidhuliwe na radiko huru, hivyo kufanya kiwanda cha mbegu za kiume kutengeneza mbegu zenye afya na zenye uwezo wa kupiga mbizi kwa kasi.
Broccoli ni aina ya mboga ambazo zipo hapa nchini ingawa si maarufu kwa Watanzania, ila katika migahawa ya Magharibi na ya Kichina, mboga hii yenye kufanana na uyoga inasifika kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha foliki ambayo hujulikana pia kama vitamin B9. Vitamin B9 ilishajulikana kwa kusaidia wanawake waliokuwa wagumba kuweza kushika ujauzito, kwa sasa pia inajulikana kusaidia wanaume wagumba.
Tunda la komamanga ambalo lipo pia katika jamii yetu linajulikana kusaidia kutengenezwa idadi kubwa ya mbegu za kiume zenye ubora.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sOlzqX
via IFTTT


Baada ya kuukosa ubingwa, Patrick Kluivert abwaga manyanga.

Baada ya kuukosa ubingwa, Patrick Kluivert abwaga manyanga.

Msimu ulioisha wa ligi pamoja na kuwekeza pesa nyingi sana katika usajili na kununua baadhi ya wachezaji wakubwa lakini klabu ya Ufaransa ya PSG ilishuhudia ikipoteza kombe la Ligue 1 ambapo kombe hilo lilienda kwa timu ya Monaco.
Patrick Kluivert alikuwa mkurugenzi wa masuala ya ufundi katika timu hiyo na ameamua kubwaga manyanga, Kluivert ambaye ameshawahi kuvichezea vilabu vya Ajax,Ac Millan na Barcelona amedumu katika ukurugenzi huo kwa muda mfupi wa msimu mmoja tu.
Haijawekwa wazi sana sababu za Kluivert kubwaga manyanga lakini inaonekana wazi wazi kwamba kitendo cha Monaco kuumaliza ubabe wa PSG na matokeo yao katika Champions League ndio sababu kubwa kwa Kluivert kuachia ngazi kwani hata mabosi wa timu hiyo hawakufurahishwa na mwenendo wa timu hiyo tangu Kluivert apewe jukumu hilo.
Raisi wa klabu ya PSG Nasser Al Khelaifi amesema kocha wa klabu hiyo Emery atabaki kuwa kocha wao lakini akimshukuru Kluivert kwa kazi aliyoifanya akiwa klabuni hapo”tunamshukuru Patrick kwa kazi kubwa aliyofanya akiwa na sisi na tunamtakia kila la kheri kwa kile alichoamua kukifanya katika miaka ijayo” alisema Khelaifi.
Msimu huu PSG wameshinda Coupe de France na Coupe de la Ligue pekee matokeo ambayo hayakuwa mazuri na yalimfanya Kluivert na kocha Unai Emery kuonekana kama wanaiangusha timu na hivyo Patrick Kluivert kuamua kuachana na timu hiyo.

from Blogger http://ift.tt/2r5fghn
via IFTTT


Mapya Kuhusu Kesi ya Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent

Mapya Kuhusu Kesi ya Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent

MAHAKAMA ya Wilaya ya Arusha, imeendelea kuahirisha kesi inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent ya mjini hapa, Innocent Mushi, hadi Julai 5, mwaka huu kutokana na upelelezi kutokukamilika.
Mtuhumiwa huyo pamoja na mwenzake ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi, Longino Nkana, wanatuhumiwa kwa makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha watoto bila kuwa na vibali muhimu.
Mushi aliburuzwa kwa mara ya kwanza Mei 12, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ambapo anakabiliwa na mashtaka manne ya usalama barabarani.
Mbele ya Hakimu Desderi Kamugisha, Wakili wa Serikali, Alice Mtenga, aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyingine kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokukamilika.
Watuhumiwa hao walikuwa wakitetewa na Wakili Method Kimomogoro ambapo Hakimu Kamugisha alikubaliana na wakili huyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 7, mwaka huu.
Awali wakisomewa mashtaka yao Mei 12, mwaka huu, Wakili wa Serikali, Rose Sule, alidai mtuhumiwa wa kwanza Mushi anakabiliwa na makosa manne wakati Nkana akituhumiwa kwa kosa moja.
Wakili Sule alidai kwamba Mushi akiwa Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vicent anatuhumiwa kuendesha gari la abiria bila ya kuwa na leseni ya usafirishaji.
Alidai kuwa Mei 6, mwaka huu katika eneo la Kwamrombo wilayani Arusha, mtuhumiwa huyo alifanya shughuli ya usafirishaji wa abiria akiwa anamiliki gari aina ya Mitsubish Rossa T. 871 BYS.
Aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa kosa la pili linamkabili mtuhumiwa huyo ni la kuruhusu kuendeshwa kwa gari bila kuwa na bima (Road Licence), ambapo Mei 6, mwaka huu aliruhusu gari hilo kuendeshwa huku akijua halina bima.
“Kosa la tatu ni kushindwa kuingia mkataba na mwajiri wake ambapo Mei 6, mwaka huu ukiwa mmiliki wa gari hilo ulishindwa kuingia mkataba wa ajira na dereva wako Dismas Joseph Gasper ambaye kwa sasa ni marehemu,” alidai Wakili Sule alipokuwa akisoma mashtaka na kuongeza:
“Mtuhumiwa unakabiliwa na kosa la nne ambalo ni la kubeba abiria waliozidi zaidi ya 13 ambapo Mei 6, mwaka huu ukiwa Mkurugenzi, Ofisa Usafirishaji na mmiliki wa Lucky Vicent ulibeba na kusafirisha abiria zaidi ya 13, kinyume cha sheria,” alidai.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rLNVU9
via IFTTT


Mwanafunzi ajinyonga kwa kukosa ada ya Chuo

Mwanafunzi ajinyonga kwa kukosa ada ya Chuo

Mwanafunzi wa Chuo kikuu huko shauri moyo Jijini Nairobi achukua hatua ya kujiua baada ya kupita wiki mbili tu tangu arudishwe nyumbani kwa kukosa ada ya malipo.
Mwanafunzi huyo anae julikana kwa jina la Fredrick Kinyanjui mwenye Umri wa miaka 22 alikua ni mwaka wa pili katika chuo cha Multimedia amekutwa amejinyonga kwenye paa la nyumba yao jana jioni.
Mkuu wa Polisi kituo cha Buruburu DCI Jeremiah Ikiao amesema kuwa wachunguzi wamebaini mwanafunzi huyo alirudishwa nyumbani siku 14 zilizopita kwa kukosa ada ya chuo.
DCI Ikiao amesema kuwa mama wa kinyanjui alikua ameenda kazini wakati mwanafunzi huyo alipojinyonga
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rLK35K
via IFTTT


Kategori

Kategori