Mabingwa watetezi wa Ndondo Cup wamechapwa Kinesi (+Picha)

Mabingwa watetezi wa kombe la Ndondo Cup Temeke Market wamechezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Makuburi SC kwenye mchezo wa Kundi G uliopigwa kwenye uwanja wa Kinesi pale maeneo ya Sinza Dar es Salaam.
Mwinyi Ally alianza kuifungia bao Makuburi dakika ya 56 kipindi cha pili baada ya timu hizo kumaliza kipndi cha kwanza bila kufungana, Paul Ndauka akaisawazishia Temeke Market dakika ya 70 lakini wakati zimesalia dakika nane tu mechi imalizike Victor Hangaya akaifungia Makuburi bao la ushindi.
Mechi hiyo ilishuhudiwa na Mbuge wa Jimbo la Ubungo Mh. Said Kubenea ambaye alikuwa mwenye tabasamu lisililo kauka usoni mwake kutokana na kushuhudia kandanda safi ambalo kwa hakika lilimburudisha.
Katika uwanja wa Mwl. Nyerere, Magomeni, Dar Police Collage wamepoteza mechi yao ya pili mfululizo kwenye Kundi G baada ya kufungwa 1-0 na Stim Tosha timu kutoka maeneo ya Mabibo. Dar Police Collage wamejiweka kwenye wakati mgumu wa kusonga mbele kwenye michuano hiyo wakiwa hawana hata pointi hadi sasa baada ya kucheza mechi mbili.
Licha ya kuwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anacheza Fanja FC kutoka falme za kiarabu lakini bado maafande hao wa Polisi wameshindwa kufurukuta kwenye michuano hiyo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tZAP41
via IFTTT