Edin Dzeko anaamini mchezaji huyu ndio bora zaidi kuwahi kucheza naye

Edin Dzeko ni kati ya washambuliaji ambao walionekana wanajua kuzifumua nyavu tangu akiwa na klabu ya Man City kutokana na wepesi wake kucheka na nyavu.
Alipohamia nchini Italia kukipiga katika klabu ya As Roma ndio moto wake umeonekana kuwa mkubwa zaidi na kuwa kati ya washambuliaji wakuogopwa katika Serie A.
Sasa Dzeko katika maisha yake ya soka amecheza na nyota wengi bora akiwemo Fransesco Totti, Kun Aguero na Yaya Toure lakini hao wote haamini kama walikuwa bora kuliko David Silva.
Dzeko amekiri na kusema miguu ya David Silva ilikuwa ina vitu vingi vitamu wanapokuwa uwanjani na hiinilimfanya yeye asichoke kumuangalia Mhispania huyo.
“Usidhani lile jina la “litle magician” aliitwa itwa tu,hapana. Yule ni liltle magician kweli kwani vitu anavyofanya akiwa na mpira vinastaajabisha hakika ni bora sana” alisema Dzeko.
Pamoja na sifa hizo lakini kocha Pep Gurdiola bado hamuamini sana Silva na ununuzi anaoendelea kufanya katika timu yake unaweza miweka kiungo huyo katika bench.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s1RO9r
via IFTTT