Dereva bodaboda afariki dunia akiwa amembeba Askari

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga leo limewatawanya madereva bodaboda zaidi ya 100 waliokuwa wanaandamana kuelekea eneo la Ibinzamata kwenye msibani kwa dereva mwenzao Joel Mamla (26) ambaye alifariki dunia jana akiwa amempakia askari wa usalama barabarani aliyekuwa amemkamata kwa kosa la kutokuvaa kofia ngumu (Helment).
Joel ambaye alikamatwa na askari waliokuwa kwenye majukumu yao ya kila siku, aliamuliwa kuelekea kituo cha polisi huku akiwa na askari amembeba kwenye pikipiki yake lakini baadaye anadaiwa kuwa alibadilisha uelekeo na kwenda Barabara ya Tinde huku akimwambia askari watakufa pamoja na kisha kuigongesha pikipiki kwenye nguzo ya alama za barabarani na baadaye kufariki dunia huku askari huyo akijeruhiwa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Jumanne Murilo, amekiri kutokea kwa tukio hilo.
“Deereva bodaboda huyo baada ya kukamatwa aliamliwa apelekwe kituoni, ndipo akambemba askari PC Edmond, lakini kabla hawajafika kitunoni, ghafla alielekeza pikipiki mahala pengine huku akimwambia askari lazima wafe wote.
“Wakati pikipiki hiyo ikiwa mwendokasi, askari huyo alianza kujihami kumzuia lakini bahati mbaya hakufanikiwa na hatimaye kusababisha ajali hiyo iliyopelekea kifo,” alisema Kamanda Murilo.
Aidha alisema baada ya tukio hilo wananchi kwa kushirikiana na bodaboda walianzisha vurugu kwa kuwarushia mawe askari polisi, ndipo jeshi hilo lilipotumia nguvu ya ziada kupiga mabomu, ili kuimarisha usalama na hali ya amani ambpo hatimye kufanikiwa kuituliza.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sGAN1h
via IFTTT