Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Steven Mengele maarufu Steve Nyerere amethibitishia umma wa Watanzania kuwa sauti inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kwake na ni kweli kuwa ni maongezi kati yake na Mama Wema Sepetu.
Steve Nyerere amesema mtu yeyote asipotoshe jambo hilo kwani yale mazungumzo aliyafanya na Mama Wema Sepetu siku tano kabla hawajatangaza kuhamia CHADEMA, na kwamba hakuwa anafahamu kama alikuwa akirekodiwa.
Nyerere ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja tu tangu Mama Wema Sepetu alipokanusha kuwa sauti inayosambazwa si ya kwake kwa sababu hata simu yake haijawashwa kutoka na ‘ubusy’ alionao pamoja na simu kuwa na matatizo.
Katika maongezi hayo anasikika Steve Nyerere akizungumza na Mama Wema Sepetu ambapo walikuwa wakijadili kuhusu kukamatwa kwa Wema kwa tuhuma za dawa za kulevya.
Mama Wema alikuwa akimuuliza Steve Nyerere kwanini hajaenda kumuona Wema Sepetu mahabusu na akitaka kujua msimamo wa baadhi ya viongozi aliowataja majina kuhusu suala la Wema kukamatwa akidai kuwa ni uonevu kwani alikipigania sana Chama cha Mapinduzi wakati wa kampeni.
Hapa chini ni maongezi kati ya Mama Wema Sepetu na Steve Nyerere.
http://ift.tt/2lzDsXh
http://ift.tt/2lOWUSg
http://ift.tt/2lzDsXh
http://ift.tt/2lOWUSg
ANGALIA VIDEO CHIDEO
from Blogger http://ift.tt/2mnRf3l
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2l9X82e
via IFTTT