Jopo la wanasheria wa kijitolea wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Ijumaa hii wametoa ripoti ya kazi waliyoifanya katika mkoa wa Dar es salaam kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu.
RC Makonda akiwatambulisha wanasheria hao Disemba mwaka jana
Wanasheria hao ambao waligawanywa katika wilaya nne, Kinondoni, Ilala, Kigamboni pamoja na Temeke waliweza kuwafikia wananchi 10,217.
Akiongea na waandishi wa habari mmoja kati ya wanasheria hao wakiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa, alisema kwa kipindi hicho kidogo wameweza kusuluhisha migogoro mbalimbali ya wananchi ambayo ilikuwa inatokea kutokana na kukosa msaada wa kisheria.
“Tumeweza kusikiliza kesi za mirathi,ndoa,ajira pamoja na migogoro ya ardhi. Kwa kesi za mirathi tuliwahi kupata malalamiko kutoka kwa msimamizi wa mirathi, amabaye zoezi lake kubwa lilikuwa ni kukusanya mali za marehemu, na alihitajika kuonyeshwa file lenye nyaraka za marehemu kutoka ofisi aliyokuwa akifanyia kazi marehemu, lakini zoezi hilo lilichukua miaka 10, kila mara alikuwa akifuatilia file hilo anaambiwa halipo. Lakini baada ya kufika ofisini kwetu tulifanya mawasiliano na akafanikiwa kuipata file hilo,” alisema Mwanasheria huyo.
Kwa upande wa RC Makonda aliwapongeza wanasheria hao huku akiwataka wanasheria wengine kujitokeza kuwasaidia wananchi ambao wanahitaji msaada wa kisheria.
ANGALIA VIDEO CHIDEO
ANGALIA VIDEO CHIDEO
from Blogger http://ift.tt/2lPU2nT
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lG8oqD
via IFTTT