WATENDAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAHIMIZWA KUSIMAMIA USAFI IPASAVYO -KATIBU MKUU TAMISEMI


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imewaagiza watendaji wa Halmashauri zote za jijini Dar es Salaam kusimamia ipasavyo suala la usafi katika maeneo mbalimbali ili kusadia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

Katika agizo hilo la Serikali ametoa  wiki mbili kwa watendaji wote kuhakikisha wanaliweka jiji katika hali ya usafi na endapo halitatekelezwa hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na watendaji wa Serikali leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, amesema kuwa utekelezaji wa malengo waliyokuwa wamejiwekea tangu  2013.

“Mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu umekuwa janga, kutokana na uchafu kukithiri katika jiji na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kuendelea kuugua,”alisema Sagini.
Pia amewataka watendaji wa halmashauri kuwatengea maeneo maalum ya kufanyia biashara, mama lishe na baba lishe badala ya kuwafukuza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasco), Mhandisi, Cyprian Luhemeja, alisema kipindupindu hakiwezi kumalizika jijini hapa kama Halmashauri hazitashirikiana na Dawassa na Dawasco.

Alisema kutoshirikiana kwa halmashauri na mamlaka za maji, kuna sababisha ujenzi holela ambao unapita katika miundombinu ya maji taka.

Pia alisema changamoto kubwa ambayo watu wengi hawaitambui ni kuhusu wasambazaji wa maji majumbani ambao ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha kipindupindu.

“Wasambazaji hawa wamekuwa wakati mwingine wanasafisha maji taka na kuyasambaza majumbani jambo ambalo linasababisha magonjwa hayo.
Kutokana na hali hiyo sisi kama DAWASCO hatutamruhusu mtu kusambaza maji kama hana kibali maalumu kilichotoka kwetu,”alisema