Usiku wa kuamkia leo October 16 2015 headlines za siasa Tanzania zimetawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).
Katika taarifa nyingine kutoka upande wa CCM iliyotolewa na naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba mida ya saa sita usiku ilisema >>> ‘Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye kampeni ziko salama‘
Baadae aliandika >>> ‘Kwakuwa ilisemekana kuwa chopa ya kampeni ya CCM imeanguka, tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa tulizokodi kama Chama hakuna iliyoanguka‘ hiyo ndio ilikua tweet ya mwisho kuandika na January Makamba usiku huo lakini badae aliRT kilichoandikwa na Waziri Nyalandu na Zitto Kabwe.
Zitto aliandika >>> ‘Naomba utulivu.1) ajali ya helkopta imethibitishwa 2) kuwaka hakujathibitishwa 3)ndugu yangu Deo alikuwamo 4)hakuna uthibitisho wa madhara, naomba utulivu mpaka tupate taarifa rasmi zilizothibitishwa na mamlaka husika, naomba sana hilo ili kuepuka sintofahamu‘