Ni mwimbaji wa bongofleva Dayna Nyange ambaye ameungana na mastaa wengine wa Tanzania kama rapper Nay wa Mitego, Timbulo, Bob Juniour, Walter Chilambo, waigizaji Shamsa Ford na Jackline Wolper kwenye kampeni za mgombea Urais waUKAWA Edward Lowassa.
Pamoja na kuonyesha wazi kuwa team UKAWA, Dayna amesema japokuwa kila mtanzania ana chaguo lake la mgombea au chama, haitakiwi ilete chuki au uadui bali kila mmoja aelewe na kuziheshimu hisia za mwenzake kisha akamilishe kiu yake kwa kupiga kura kwa amani na utulivu na kuendeleza sifa ya amani iliyokuwepo kwa kitambo’
Dayna amesema >>> ‘Kila Mtanzania ana haki ya kufanya kile nafsi yake inachoamini sio kwa kulazimishwa, mimi naamini ninachokifanya nafsi yangu imeridhika naamini niko huru na sehemu ambayo ina amani, siwezi kukuchukia sababu eti wewe upo CCM mimi niko UKAWA….. hapana, hata ninapokuwepo kwenye kampeni simlazimishi mtu kuja UKAWA, ninachofanya ni kuwaelewesha watu tu wakielewa sawa….‘
‘Sisi ni Watanzania ambao tunahitaji amani na upendo.. tuelimishe Watanzania tumuachie mwenyenzi Mungu na Watanzania wafanye maamuzi, hata kama kuna shabiki ambaye hayuko upande wangu hilo sio tatizo langu wala lake na wala sio tatizo, ni uhuru wa maamuzi yake… anaweza kuniweka pembeni kwenye huu muda wa uchaguzi, uchaguzi ukiisha tutakutana kwenye stage‘ <<< Dayna