Usafiri wa Ndege ni moja ya usafiri ambao kwa sasa unazidi kuwa nafuu na pia wa haraka ambao watu wengi hupendelea kuutumia… kwa mfano badala ya kusafiri Dar es salaammpaka Kigoma kwa basi ili kuepusha kuumia muda mwingi kama ilivyo zamani kwa sasa ni rahisi na haraka kwa kutumia usafiri wa anga.
Ni jambo la kawaida kwa sasa kwa kila Mkoa kuwa na uwanja wa Ndege, moja ya mikoa yenye viwanja vya ndege ni pamoja na Mkoa wa Kigoma.
Uwanja huu unatumika na watu mbalimbali wakiwemo wageni wanaotoka nje ya nchi… Uwanja upo Kigoma Mjini maeneo ya Katubuka