Mkazi wa Kijiji cha Nyamatongo, wilayani Sengerema, Mwanza, akiwa amevaa kichwani  mfano wa karatasi la kupigiwa kura lenye picha ya Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk John Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan. Dk Magufuli alihutubia mkutano wa kampeni katika Kijiji hicho.
Dk Magufuli ameahidi kujenga viwanda vya kukamua juisi za mananasi yanayolimwa kwa wingi mkoani Geita ili kuongeza thamani ya zao hilo pamoja na kufufua viwanda vya pamba.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Wananchi wa Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli ambaye akizungumza nao aliahidi kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Sengerema hadi Nyahunga.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi alipowasili Gati la Kamanga wilayani Sengerema.
 Mmoja wa wananchi akishangilia kwa furaha baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika eneo la Kamanga, Sengerema.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi waliomzuia asipite katika Kijiji cha Katunguru, Sengerema.
 Wananchi wa Kijiji cha Kasenyi wakimshangilia Dk Magufuli na kuahidi kumpigia kura za ndiyo.
 Mmoja wa wakazi wa Kasenyi akiwa amevaa kichwani karatasi la mfano la kuwapigia kura wagombea wa CCM, Dk Magufuli na Smia Suluhu Hassan wakati wa mkutano usio rasmi katika Kijiji hicho.
 Dada akimshangilia Dk Magufuli huku akiwa amevaa karatasi  za mfano wa kupigia kura viongozi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Jumapili.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dk Magufuli katika Mji wa Nyahunga, Jimbo la Buchosa, Senegerema.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema, Charles Tizeba wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Nyahunga.
 Wananchi wa Kijiji cha Nzera, Geita Vijijini wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli.
 Moja ya mabango yaliyokuwepo kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Nkoma, Geita Vijijini.
 Akiwa na furaha baada ya kumuona Dk Magufuli katika Kijiji cha Nzera, Geita Vijijini.
 Dk Magufuli akimnadi kwa wanachi Mgombea ubunge Jimbo la Geita Vijijini kupitia CCM, Joseph Musukuma katika Kijiji cha Nzera.
 Wasanii Temba na Chegge wakitumbuiza wakati wa mkutano huo.
 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea ubunge Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Nkoma.
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma.
 Wasanii wakishangilia katika mkutano huo uliohutubiwa na Dk Magufuli.
 Msukuma akimuombea kura za ndiyo Dk Magufuli.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.