Uganda yapoteza wanajeshi 12 nchini somalia



Wanajeshi wa Uganda katika kikosi cha AMISOM nchini Somalia
Wanajeshi wa Uganda katika kikosi cha AMISOM nchini Somalia
 
makala zinazohusiana
Uganda ilithibitisha wanajeshi wake 12 walio katika mamlaka ya kikosi cha AMISOM waliuwawa baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab kushambulia kituo cha jeshi la Umoja wa Afrika katika mji wa Janale, kusini mwa Somalia siku ya Jumanne.
Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda alisema katika mtandao kwamba miili 10 ilisafirishwa kutoka Mogadishu kwenda Uganda Alhamisi. Bwana Ankunda alisema AMISOM iliwatambua  wanajeshi wote na hakuna mwanajeshi aliyepotea kutoka kituo cha Janale, kilichopo kilomita 120 kusini-magharibi mwa Mogadishu.
Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab huko Somalia
Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab huko Somalia
Wanamgambo wa Al-Shabaab walidai kiasi cha wanajeshi wa Uganda 70 waliuwawa katika shambulizi la Jumanne lakini vyanzo vya Sauti ya Amerika-VOA vilisema jumla ya idadi ya vifo vya wanajeshi ni 20.
Msemaji huyo wa jeshi la Uganda alisema “shambulizi hilo limebadili mtazamo” na al-Shabaab watarajie “majibu muafaka” kutoka kwa wanajeshi wa Uganda. Bwana Ankunda aliongeza kwamba licha ya shambulizi, “Uganda haitasitisha  juhudi zake za kusaidia kuleta amani nchini Somalia”.
Wakati huo huo mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Uganda, Jenerali Edward Wamala alitembelea wanajeshi  wa mstari wa mbele katika mji wa Janale mahala ambapo alikutana na UDPF na  kuwapongeza kwa azma yao ya mapambano wanayofanya  dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab ambao walishambulia kituo hicho.