Showing posts with label habari na voaswahili. Show all posts
Showing posts with label habari na voaswahili. Show all posts
Marekani na Ulaya kuingilia mzozo wa Congo.

Marekani na Ulaya kuingilia mzozo wa Congo.


Raiya wa Congo akiandamana kupinga uamuzi wa rais N'Guesso wa kujiongeza muda wa kuhudumu.
Raiya wa Congo akiandamana kupinga uamuzi wa rais N'Guesso wa kujiongeza muda wa kuhudumu.
Makundi ya upinzani na ya kiraia kutoka Jamhuri ya Congo yamekutana Alhamisi na wawakilishi kutoka Marekani na Ulaya ili kuzungumzia kuhusu hali ya kisiasa nchini humo, ambapo kura ya maoni inayokusudia kumruhusu rais kuwania muhula wa tatu madarakani imezusha ghasia za kisiasa.
Perfect Kolelas, kiongozi wa chama cha upinzani cha Congolese Movement for Democracy and Integral Development, amesema ajenda zinajumuisha mashauriano ya kusaidia kumaliza ghasia za kisiasa nchini humo ambazo zimesababisha vifo vya watu wane siku ya Jumanne.
Kolelas ameiomba jumuiya ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Afrika kuingilia kati ili kuhakikisha katiba haikiukwi.
Vyuo vikuu zaidi ya 10 vyafungwa kwa muda Afrika kusini

Vyuo vikuu zaidi ya 10 vyafungwa kwa muda Afrika kusini


Makundi ya watu wakiandamana  Johannesburg, South Africa.
Makundi ya watu wakiandamana Johannesburg, South Africa.
Karibu vyuo vikuu 14 vya Afrika kusini vimefungwa kwa muda wakati wa kuongezeka kwa wimbi la malalamiko na maandamano ya wanafunzi   kutokana na mapendekezo ya kuongezwa kwa ada. Maandamano hayo yamepelekea mapambano Jumatano kati ya wanafunzi na polisi nje ya bunge huko Capetown.
Malalamiko yalianza wiki iliyopita katika chuo kikuu cha Witwatersrand huko Johannesburg baada ya mapendekezo ya ongezeko la asilimia 10. Toka wakati huo ujumbe wa Twitter “ada lazima ipungue”umesambaa kwenye mitandao ya kijamii  na malalamiko yametapakaa katika taasisi tofauti ikiwa ni pamoja na chuo kikuu mashuhuri cha Capetown, chuo  kidogo cha kiliberali Rhodes na kile cha nje ya mji Fort Hare.
Maandamano hayo yamelazimisha viongozi wa vyuo vikuu kukutana wiki hii na waziri wa elimu ya juu na mafunzo Blade Nzimande katika jaribio la kutafuta suluhu.
Jeshi la polisi Tanzania lasisitiza amani wakati wa uchaguzi

Jeshi la polisi Tanzania lasisitiza amani wakati wa uchaguzi


Ernest Mangu mkuu wa jeshi la polisi nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo amesema kwamba jeshi hilo halitasita kukabiliana na watu au kikundi chochote kitakachokaidi sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi kwa kisingizo cha kulinda kura.
Mkutano wa kampeni za uchaguzi Tanzania
Mkutano wa kampeni za uchaguzi Tanzania
Nchini Tanzania wakati kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kutaka tafsiri ya sheria juu ya umbali unaoruhusiwa wapiga kura kusimama  baada ya kupiga kura haijatolewa uamuzi,  jeshi la polisi nchini humo limesisitiza kwamba halitaruhusu kuwepo mikusanyiko yoyote baada ya upigaji  kura kukamilika Oktoba 25 mwaka huu
Jaji Sakieti Kihiyo, ambaye ni kiongozi wa jopo la majaji watatu leo aliahirisha  tena hukumu ya kesi hiyo katika shauri  la kikatiba linaliloleta mvuto wa aina yake nchini humo lililofunguliwa na mgombea Ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chadema, Amy Kibatala, akiomba mahakama kutoa tafsiri ya kifungu cha 104 cha sheria ya uchaguzi baada ya kauli mbalimbali za viongozi wa Serikali kutoruhusu wapiga kura kukaa vituoni mara bada ya kumaliza kupiga kura huku wapinzani wakisisitiza kuwa sheria inaruhusu kukaa umbali wa mita mia mbili
Ernest Mangu  mkuu wa jeshi la polisi  nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo amesema kwamba jeshi hilo halitasita kukabiliana na watu au kikundi chochote kitakachokaidi sheria, kanuni na taratibu  za uchaguzi kwa kisingizo cha kulinda kura.
Mkuu huyo wa jeshi la polisi ametaka kuwepo kwa amani na utulivu kama ilivyokuwepo wakati wote wa kampeni za uchaguzi mkuu zinazohitimishwa Jumamosi Oktoba 24 mwaka huu
Watanzania wanatarajiwa kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kuwachaguwa madiwani, wabunge na rais, katika uchaguzi mkuu ambao vyama vinane vimesimamisha wagombea wa urais.
Tume ya uchaguzi Tanzania yatakiwa kuweka wazi taratibu zake

Tume ya uchaguzi Tanzania yatakiwa kuweka wazi taratibu zake

Baadhi ya vifaa vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Baadhi ya vifaa vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Taasisi za haki za binadamu nchini Tanzania zimetahadharisha masuala kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo ambapo walisema yanaweza kuleta migogoro kwa wananchi na vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Kituo cha sheria na haki za binadamau LHRC kilizungumzia hatua ya tume ya taifa ya uchaguzi ya kutoweka hadharani daftari la kudumu la wapiga kura wakati huu ambapo zimebaki siku 18 tu ili watanzania waweze kupiga kura hapo oktoba 25 mwaka huu.
Jaji Damian Lubuva
Jaji Damian Lubuva
Hivi karibuni mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania,  jaji mstaafu Damian Lubuva alikaririwa akisema kwamba hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kuandaa daftari la kudumu la wapiga kura tayari kwa kuliweka hadharani siku kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi jambo ambalo limeshalalamikiwa na baadhi ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Wanaharakati wa haki za binadamu pia wamehoji tume ya taifa ya uchaguzi pia kuchelewa  kutoa orodha ya vituo vya kupigia kura  pamoja na jitihada za wadau wa uchaguzi zikiwemo asasi hizo za kiraia za kutaka kupata orodha hiyo.

Asasi za kiraia nchini Tanzania pia ziliiomba serikali kutobadilisha watendaji na makamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi wakati huu zikiwa zimebaki siku chache kufikia tarehe ya uchaguzi mkuu ili kuondoa dhana potofu kwamba inajaribu kuweka mazingira ya kuwezesha chama tawala cha CCM kushinda uchaguzi huo.

Kategori

Kategori