Ernest Mangu mkuu wa jeshi la polisi nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo amesema kwamba jeshi hilo halitasita kukabiliana na watu au kikundi chochote kitakachokaidi sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi kwa kisingizo cha kulinda kura.
Nchini Tanzania wakati kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kutaka tafsiri ya sheria juu ya umbali unaoruhusiwa wapiga kura kusimama baada ya kupiga kura haijatolewa uamuzi, jeshi la polisi nchini humo limesisitiza kwamba halitaruhusu kuwepo mikusanyiko yoyote baada ya upigaji kura kukamilika Oktoba 25 mwaka huu
Jaji Sakieti Kihiyo, ambaye ni kiongozi wa jopo la majaji watatu leo aliahirisha tena hukumu ya kesi hiyo katika shauri la kikatiba linaliloleta mvuto wa aina yake nchini humo lililofunguliwa na mgombea Ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chadema, Amy Kibatala, akiomba mahakama kutoa tafsiri ya kifungu cha 104 cha sheria ya uchaguzi baada ya kauli mbalimbali za viongozi wa Serikali kutoruhusu wapiga kura kukaa vituoni mara bada ya kumaliza kupiga kura huku wapinzani wakisisitiza kuwa sheria inaruhusu kukaa umbali wa mita mia mbili
Ernest Mangu mkuu wa jeshi la polisi nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo amesema kwamba jeshi hilo halitasita kukabiliana na watu au kikundi chochote kitakachokaidi sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi kwa kisingizo cha kulinda kura.
Mkuu huyo wa jeshi la polisi ametaka kuwepo kwa amani na utulivu kama ilivyokuwepo wakati wote wa kampeni za uchaguzi mkuu zinazohitimishwa Jumamosi Oktoba 24 mwaka huu
Watanzania wanatarajiwa kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kuwachaguwa madiwani, wabunge na rais, katika uchaguzi mkuu ambao vyama vinane vimesimamisha wagombea wa urais.