Polisi Garisa yakamata watu wanne wakitaka kujiunga na Al-shabaab


Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab ambalo linashutumiwa kuwalaghai vijana kujiunga na kundiKundi la wanamgambo wa Al-Shabaab ambalo linashutumiwa kuwalaghai vijana kujiunga na kundi
Polisi nchini Kenya walisema wamewakamata watu wanane kwa shutuma za jaribio la kujiunga na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab la nchini Somalia. Maafisa wa Garissa walisema wanaume hao wanane walikamatwa katika mji wa Dadaab hapo Jumatatu.
Mratibu wa kieneo wa amani na usalama, Mohamud Ali Saleh alisema watu hao wanatokea nchini Tanzania. Hakutoa maelezo zaidi.  Bwana Saleh alisema polisi pia wamewakamata wanawake wawili wiki iliyopita katika jimbo la kaskazini-mashariki. Alisema wanawake hao mmoja raia wa Kenya na mwingine raia wa Tanzania walichukuliwa kuandikishwa kama wake katika kundi la Al shabab.