Mkuu
wa vipindi channel ya A & E Networks, Racheal Job akizungumza na
waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa
kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za
DStv na GoTv kupitia MultiChoice nchini Mauritius. Katikati ni
Mkurugenzi wa Kanda channel ya A & E Networks, Anthea Petersen na
kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah
Williams-Robbins.
Mkuu
wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins
akifafanua jambo kwenye jukwaa lililowakutanisha waandishi wa habari
(hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika nchini Mauritius.
Ebenezer Donkoh kutoka YFM Ghana akiuliza swali katika mkutano wa waandishi wa habari ulionadaliwa na MultiChoice Africa.
Philip
Mwaniki kutoka Nairobi, Kenya akiuliza swali kwenye jukwaa hilo
lililowakutanisha waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika
waliohudhuria wanaohudhuria kongamano hilo linalotarajiwa kumalizika leo
nchini Mauritius.
Na Mwandishi Wetu
DOKUMENTARI
inayomhusu mmoja wa masupastaa ambaye kadhia yake ya mauaji ilitagazwa
sana OJ Simpson itarushwa na na chaneli ya uhalifu na uhunguzi ya A and E
Networks Oktoba mwaka huu.
Dokumentari
hiyo inatolewa katika siku ya kumbukumbu ya miaka 20 ya hukumu ya moja
ya kesi iliyoandikwa sana na vyombo vya habari vya Marekani.
Doukumentari
ya kwanza ya The Secret Tapes of the O.J. Case: The Untold Story
(itarushwa Oktoba 6, saa 21) na O.J. Speaks: The Hidden Tapes
(itakayorushwa Oktoba 13 saa 21).
Dokumentari
hizo zimesheheni mambo ambayo hayajajulikana kwa watu ambayo
yalizungumzwa na OJ Simpson na wengine waliohusika katika tuhuma za
mauaji wakati wa shauri la jinai la la kiria.
Imeelezwa
nchini Mauritius kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali
vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice
kwamba dokumentari hizo ni zenye msisimko mkubwa katika msimu ujao wa
A+E Networks.
Mkurugenzi
wa A+E Networks wa Kanda ya Afrika, Anthea Petersen : “msimu huu A+E
Networks inaringia kitu kikubwa kitakachoingia sokoni cha OJ Simpson kupitia dokumentari za uhalifu na uchunguzi ( CI).”
Petersen pia alisema kwamba hivi karibuni wamefungua ofisi ya A+E Networks’ jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mkurugenzi
huyo wa A+E Networks kanda ya Afrika amesema kwamba wanawekeza katika
bara la Afrika kama chaneli bora ya burudani wakiwa na upenzi wa
asilimia 50 katika robo ya kwanza.
Aidha anazungumzia ujio wa programu ya Lifetime kuanzia Oktoba 16 mwaka huu itakayokuwa hewani saa 2 na dakika 50.
Kuna programu inayokwenda kwa jina la Four Weddings SA ambayo kwa sasa ndiyo inayowika na ipo kila Ijumaa.
Pia
kuna kitu kizuri ndani ya HISTORY ambayo imepata haki miliki ya
kutangaza filamu isiyokuwa na skrpti ya Idris Elba: Mandela, My Dad
& Me, baada ya kucheza Mandela: Long Walk to Freedom.
Pia
kuna shoo ya Fifth Gear ndani ya chaneli ya HISTORY, huku wakiwa na
vitu vya mvuto safi kabisa kuhusu barabara za Afrika Kusini.
Mambo mengine matamu ni kama Pawn Stars SA, ikiwa katika msimu wa pili ndani ya History ityakayoanza kuonekana mapema mwakani.