Waandishi wa habari wahimizwa kuandika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

WANAHABARI Nchini wametakiwa kuwa mabarozi wa uandishi wa habari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuiokoa dunia na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayo tokea kwa kasi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya hali ya hewa wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dr. Ladislaus Chang’a wakati wa kutoa elimu kwa baadhi ya wakulima, wapima nvua na waandishi wa habari Mkoani Njombe.

Alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuhakikisha kila mara wanawakumbusha wananchi kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na madhara yake.

Alisema kuwa katika kipindi hiki waandishi wasipo wakumbusha wananchi mara kwa mara juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi mazingira yataendelea kuharibika, na joto kuongezeka maradufu.

Alisema kuwa baadhi ya wananchi hawajui juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kuwa mafuriko na kukosekana kwa mvua kunatokea kutokana na kuwapo kwa upotevu wa misitu na ongezeko la moshi kutoka katika magari na viwanda duniani.

Chang’a alisema kuwa waandishi waandike habari za uharibifu wa mazingira, vyanzo vya maji na madhara yake ili wananchi kuelewa na kuendeleza kupanda miti pasipo kukata miti.

Aidha nao waandishi walilalamikiwa kubandwa na wamiliki wa vyombo vya habariu kwa kupewa mda mchache kwa mambo ya kutoa elimu kwa uma huku wakitoa ushauri kwa mamlaka kubadilisha mfumo wa utoaji wa taarifa za utabili wa hali ya hewa.

Raymond Francis alisema kuwa mamlaka inatakiwa kubadilisha mfumo wa kutoa taarifa hizo kwa kuzirainisha ili kupata watu wanao zifuatilia kwa wingi kuliko zinavyo tolewa na mda wa kutoa taarifa hizo.  

Francis alisema; “Mamlaka inavyo toa taarifa inatoa taarifa ngumu watanzania wengi wanapenda vitu raini, nawashauri mgetumia watu wa vichekesho watu wengi wangesikiliza, pia mda mlio weka wengi wanacheza na rimoti za runinga zao kwa kuangalia vipindi vingine ingrpendeza kabla ya taarifa ya habari au katikati ili watu kuziona taarifa hizo,” alisema.