Rais wa Syria alaumu mataifa ya nje


Rais akiwa kwenye ofisi yake amesema azimio la mgogoro wa kisiasa wa Sryria litafikiwa tu endapo nchi za nje zitaacha juhudi za kukandamiza serikali yake.
wakimbizi wa Syria wakivuka mpaka kutoroka ghasia nchini mwao.
wakimbizi wa Syria wakivuka mpaka kutoroka ghasia nchini mwao.
Rais wa Syria, Bashar al-Assad amelaumu mataifa ya nje kuingilia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa  miaka minne nchini mwake kwa kusema hatoruhusu waangalizi wa kimataifa katika uchunguzi wowote ujao.
 Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Al-Manar, ambacho kinaendeshwa na kundi la wanamgambo wa Hezbollah, Bwana Assad alisema hapana kwa waangalizi wa kimataifa akidai huko ni kuingilia himaya ya  Syria.
Shirika la habari la Associated Press limeripoti kwamba, Bwana Assad aliongeza kusema kwamba ni chombo gani cha kimataifa ambacho kimepewa mamlaka ya kutoa cheti cha ufanyaji kazi mzuri.
Akionekana  katika ofisi ya Rais mjini Damascus, amesema azimio la mgogoro wa kisiasa wa Sryria litafikiwa tu endapo nchi za nje zitaacha juhudi za kukandamiza serikali yake.