Mch. Mtikila awasema Ukawa




MWENYEKITI wa chama cha DP Maendeleo Mch. Christopher Mtikila amesema kuwa Umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ni wasaliti na wamekuwa vipande 30 vya fedha na kuwasaliti wananchi.


Alisema kuwa Ukawa walikula vipande 30 vya fedha na kuwa hawajawahi kukanusha kuwa walikubaliana kuhusu katiba ya wananchi Pendekezwa ya Watanzania kila Rais anavyo zungumza na waandishi wa habari mwisho wa mwezi anasema kuwa anawashangaa ukawa na kuwa walikubaliana kuhusu katiba lakini ukawa hawatoi tamko la kukanusa.


Aliyasema hayo akiwa Mkoani Njombe wakati Akizungumza na wanachama wa chama hicho na kusema kuwa ukawa wamekula vipande vya fedha na kuwasaliti wananchi na hasa kuhusiana ana katiba Pendekezwa ambayo ilisababisha kuundwa kwa Umoja huo na kuwa yeye akiwa ni mmoja wa waanzilishi.

Alisema kuwa wananchi wamesalitiwa na Umoja huo kwa kuwa umekaa kimya kila Rais anapo zungumza na wananchi mwisho wa mwezi na kusema kuwa anawashangaa ukawa na kuwa walikubaliana.

“Rais anapo zingumza na waandishi wa habari kila mwisho wa mwezi anasema kuwa anawashangaa ukawa kwa kuwa walisha malizana,” alisema na kuongeza.

“Ukawa walikutana na Rais na kupewa pesa huko na kuondoka usiku wa manane na kuwanyamazisha kisha kila mmoja kumsindikiza nyumbani kwake na mzigo wa pesa aliopewa,” aliongeza Mch. Mtikila  

Aidha Mch. Mtikila alisema kuwa kuna wanasheria wanao shugulikia tatizo la kuondolewa katika kinyang’anyilo cha ugombea wa uraisi na kusema kuwa kuna majaji wanao shughulikia suala lake kwa hati ya dharula na kuupeleka tume ya uchaguzi.

Akisimulia mkasa na jinsi alivyo katwa alisema kuwa mgombea mwenza alishindwa kufika kwa wakati baada ya mkewe kupata mshituko na kwenda naye hospitalini.

Alisema mgombea mwenzake baada ya kupata nafuu aliwaambia kuwa atakuja na Mtikila akaomba kuwa atachelewa kidogo mgombea mwenzake na mahakamani aliapishwa  na kuwa baada ya mgombea wenzake huyo kutumiwa tiketi ya ndege alichelewa ndege na kwenda kupanda meli ya Express na kufika kwa kuchelewa.

Alisema kuwa baada ya kuwasilisha suala lake kwa mahakamani alisema kuwa mawakili waliwasilisha hilo na kuiambia tumekuwa alichelewa kwa bahati mbaya lakini tume iliikata fomu yake.

Alisema jana mawakili wake wanaendelea vizuri na wamepeleka hati ya dharura kwaajili ya kuirudisha jina lake kugombea nafasi ya urais.

Alisema kuwa anaimani jina lake lekirejeshwa atashina na kusema kuwa wagombea urais wote ni mafisadi na kuwa mwaka huu CCM wamesimamisha marais wawili kama alivyosema Mwenyekiti wa chama wananchi (CUF) Ibrahim Lipumba.

Alisema kuwa mgombea wa urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kugombea kupitia Ukawa ameshindwa CCM na ndio maana amehamia  huko baada ya kukosa nafasi katika chama hicho.