KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina la Buhula Ngassa (46) mkazi wa kijiji cha Chikobekatika Kata ya Nyachiluluma Wilayani Geita, amekamtwa na viongzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani humo, akiwa na shahada 43 za kupigia kura.
Tukio la kukamatwa kijana huyo limetokea jana majira ya saa kumi jioni wakati kijana huyo alipokuwa katika duka moja la vifaa vya elimu "stationery" akiwa anatoa nakala ya vitambulisho hivyo.
Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Busanda, George Kwacha pamoja na Mwenyekiti wa tawi la Bugambelele, Daniel Musa wameeleza jinsi walivyomkamta na kumfikisha katika kituo cha polisi Katoro.
Hata hivyo, mtuhumiwa amedai kuwa shahada hizo zilikuwa za wateja wake waliofika kusajili simu zao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo akikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa alikutwa na shahada zilizopita muda wake 7 na nyingine mpya 36 zilizotengenezwa kwa BVR. Uchunguzi zaidi unafanyika ili kufahamu malengo ya kijana huyo.