Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) pichani leo jioni imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili Wenyeji wao Tanzania Timu ya (Taifa Stars) mchezo utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakibadilishana Mawazo wakati Wachezaji wa Malawi wanajifua mara ya mwisho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo.
Tiketi za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum.
Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo.
Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi.
Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.
Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.
Baadhi ya Viongozi wa Soka wakiteta jambo Uwanjani hapo CCM Kirumba