Mbunge wa Busega achangisha milioni 13.6 kwaajili ya shule

Mbunge wa Busega Dk.Titus Kamani ameendesha Harambee kwa ajili ya ujenzi wa shule nyingine katika kijiji cha Bulima, ili kuondoa adha ya wanafunzi wanaorundikana katika shule ya msingi Nyashimo iliyopo katika kijiji cha Bukabile ambapo kiasi cha shilingi Milioni 13.6 kimepatikana.
Akihutubia katika harambee hiyo mbunge wa jimbo la busega ambaye pia ni waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi dokta Titus Kamani ameitaka kamati ya ujenzi wa shule hiyo, ambao tayari umeshaanza wautumie mchango ulitokana na harambee hiyo kwa kile kilichokusudiwa na siyo vinginevyo, ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi wawekeze kwenye elimu kwa kusomesha watoto wao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Lukale, amewapongeza wananchi hao kwa uamuzi wao mzuri wa kujenga shule hiyo na kusisitiza kuwa elimu ndiyo msingi wa maisha.

Related Posts