Benki ya Posta Tanzania TPB imetoa Taarifa yake ya Utendaji kwa mwaka 2014 ambapo kwa mara kwanza katika historia yake Benki hiyo imepata faida ya shilingi Bilioni 10 kabla ya kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo bwana Sabasaba Moshingi amesema Benki yake imefanikiwa kukuza mikopo kwa asilimia 59, ikiwa ni pamoja na kubuni bidhaa nyingine za Kibenki na kuimarisha huduma kwa wateja.
Kwa upande wa huduma kwa jamii, Benki hiyo ilitenga kiasi cha shilingi Milioni 150,ambazo zilitumika katika kusaidia shughuli mbalimbali katika sekta za Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii
