Watu zaidi ya 5,000 wafa Nepal, huku vikosi vya uokozi waendelea kumiminika


Makundi ya uokozi yanaendelea kuingia katika miji na vijiji ambavyo vinasubiri msaada nchini Nepal, ikiwa ni siku nne baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Jumamosi iliyopita.
Idadi ya vifo imefika zaidi ya 5,000, wakati watu 10,000 wakijeruhiwa. Mamia ya maelfu ya watu nchini Nepal wamechwa bila makaazi baada ya nyumba zao kuharibiwa katika janga hilo.
Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 415 ili kuisaidia serikali ya Nepal katika juhudi zake za kuwapa watu makaazi, chakula, maji na huduma za afya katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani - WFP limeonya kuwa itachukua muda kwa chakula na bidhaa nyingine kuzifikia jamii za vijijini ambazo zimeathirika kutokana na maporomoko ya ardhi.

Na Magic Fm

Related Posts