Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Akizungumza Katika Mkutano Mkuu wa NJOCOBA wa Wanahisa
MKUU wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa huo kuhakikisha zina ushirikiano mzuri kwa benki ya wananchi Njombe kwa kuwa ndio inayo saidia wananchi wenye halmashauri hizo kwa mikopo ya kilimo.
MKUU wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa huo kuhakikisha zina ushirikiano mzuri kwa benki ya wananchi Njombe kwa kuwa ndio inayo saidia wananchi wenye halmashauri hizo kwa mikopo ya kilimo.
Akizungumza katika mkutano wa wanahisa wa benki ya wananchi
Njombe (Njocoba) mkoa wa Njombe alisema kuwa benki hiyo ni ya wananchi mkoa huo
hivyo halmashauri zinatakiwa kuwa na ushirikiano na benki hiyo ili kuimalisha
benki inayo wasaidia wananchi wa halmashauri zao.
“Ras fuatilia wakurugenzi wa halmashauri ambao hawana
ushirikiano wa kweli na benki hii ya wananchi wao kwa sababu ndio inayo wapatia
wakulima mikopo na kuinua halmashauri zetu,” alisema Dkt. Nchimbi.
Alisema kuwa haitapendeza halmashauri haina ushirikiano wa
kweli na benki inayo wasaidia wakulima na wakazi wa halmashauri zao.
Alitaka benki hiyo kuwalea wakulima wao ambao wanakopa
kutitia benki hiyo na hasa kwa kuwapatia elimu ya mikopo ili kukabiliana na
tatizo la kuto lejesha mikopo kwa wakati.
Alisema kuwa benki inatakiwa kuwa ya tofauti na benki
zingine zote na hasa kwa kuwa na dawadi la wakulima ili kutoa elimu kwa
wakulima wanaokopa mikopo na kujua matumizi sahihi ya mikopo yao.
Alisema kuwa haitapendeza kuona mkopaji wa mkopo anakopa pesa
na kuzipeleka katika mambo ambayo hayakuwepo katika malenho yake ili kulina na
uulejesha kwa wakati.
Nchimbi alisema kuwa dawati hilo litasaidia wananchi kulina
mkopo kwa kuto peleka mikopo yao katika harusi, Kicheni pani na michango ya
sherehe kwa kuwa michango hiyo haileti Maendeleo.
“Kuna watu wanakopa mikopo katika kicheni pati kwa kulenga
kuwafuraisha watu walio waalika na kujikuta wakishindwa kulejesha kwa kuwa
harusi haziwezi kuzarisha,” aliongeza Nchimbi.
Aliongeza kuwa benki ili kuwa na ukuaji na kuongeza wateja
ni lazima ikawa inatoa ajira kwa wazawa wa mkoa wa Njombe ili kusaidia kuongeza
wanachama kwa kuona watoto wao wanafanya kazi benki hiyo na kujiunga kuliko
kuajiri watu kutoka nje ya mkoa wa Njombe na wakazi wa mkoa wa Njombe wataona benki
hiyo ni yao.
Aidha akisoma taarifa ya benki hiyo Menyekiti wa bodi Yohana
Kalinga, alisema kuwa benki hiyo
inapambana na wadaiwa sugu ambao hawajalejesha mikopo ili kuhakikisha benki
hiyo inasonga mbele na kuwa mikopo isiyo rejeshwa huathiri ukuaji wa benki.
Alisema kuwa anaomba halmashauri za mkoa wa Njombe kuwa na
ushirikiano na benki hiyo ili kuhakikisha kuwa benki hiyo inaimalisha wananchi
wanao jiunga kila siku ka mikopo ya kilimo.