1559: Mfalme Henry II apata majeruhi
MFALME Henry II wa Ufaransa (31 Machi 1519 – 10 Julai 1559) alipata majeruhi yalisababisha kifo chake katika mchezo wa ‘Jousting’ wakati akipambana na Gabriel de Montgomery. Mchezo wa ‘Jousting’ ulisimamishwa tangu kufa kwake nchini Ufaransa. Mchezo huo huwakutanisha wapanda farasi ambao hupambana katika mapigo ya ‘martial’.