Watu watatu wauwawa Mandera, Kenya


Kenya imeshuhudia mashambulizi kadhaa yaliyoshukiwa kuwa ya kigaidi ikiwemo lile la Westgate Mall, September 21, 2013.
Kenya imeshuhudia mashambulizi kadhaa yaliyoshukiwa kuwa ya kigaidi ikiwemo lile la Westgate Mall, September 21, 2013.
Shambulizi  jingine linaloshukiwa kuwa la kigaidi lilitokea Ijumaa katika mji wa Mandera uliopo kaskazini mashariki mwa Kenya na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo maafisa wa polisi wawili na watu saba walijeruhiwa.  
Ingawa hakuna kundi lolote la kigaidi linalodai kuhusika  na shambulizi  hilo, watu hao watatu waliofariki walikuwa kwenye msafara wa gavana wa jimbo la Mandera, bwana  Ali Roba walipokuwa wakirudi kazini baada ya shughuli za kikazi.  Habari zaidi zinasema gari moja limeharibiwa kabisa kwenye shambulio hilo.
Duru za kiusalama zinasema shambulio hilo limetokea karibu sana na barabara ya Arebia ambapo abiria wasiopungua 28 waliuwawa mwezi Novemba mwaka jana ndani ya basi lililokuwa safarini kurudi mjini Nairobi kutoka mji wa Mandera.
Katika shambulio hilo la mwaka jana kundi la wanamgambo wa al-Shabab la nchini Somalia lilidai kuhusika  na tukio hilo.
Taarifa juu ya shambulizi la Ijumaa zilisema gavana Robo hakujeruhiwa kwa sababu gari lake lilikuwa limeshapita wakati tukio likitokea.
Shambulizi la mwaka jana mjini Mandera, Nov. 22, 2014.Shambulizi la mwaka jana mjini Mandera, Nov. 22, 2014.
Wakazi wa mji wa Mandera walisema mji huo umejaa wasiwasi wa mashambulizi ya aina hiyo yanayohusishwa na ugaidi ambayo huwakumba watu wa jamii zote yaani wakristo na waislam.
Kenya  imeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara yanayosababisha vifo yakidaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia kufuatia Kenya kupeleka wanajeshi wake nchini humo ili kuisaidia serikali ya Somalia  kupambana na wanamgambo hao wanaodumaza hali ya usalama nchini hum
o