LEO KATIKA HISTORIA: Machi 27

1972: Jimmy Floyd Hasselbaink azaliwa

Tony Rominger
Nyota huyu wa Uholanzi na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea alizaliwa Paramaribo nchini Suriname ikiwa ni sehemu ya utawala wa wadachi katika bara la Amerika Kusini. Kwa sasa ni kocha wa klabu ya Burton Albion inayoshiriki ligi daraja la pili nchini England. Alianza soka lake katika vilabu vya Telstar na AZ Alkamaar. Alijiunga Chelsea akitokea Atletico Madrid alikofunga mabao 24 katika mechi 34. Aliposhuka darajani Magharibi mwa London alitupia mabao 69 katika mechi 136. Msimu wa 1998/99 alitwaa kiatu cha ufungaji bora EPL.

1974: Gaizka Mendieta azaliwa
Kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika runinga, alizaliwa Bilbao nchini Hispania ambako aliitumikia klabu ya Valencia kabla ya kutimkia Middlesbrough ya England. Anafahamika katika ulimwengu wa soka kwa ukabaji, uwezo wa ku-tackle na kutengeneza mabao. Ameitumikia La Roja akicheza mechi 40 zikiwemo za Kombe la Dunia na Michuano ya Mataifa ya Ulaya. La Liga alicheza mechi 263 na kutupia mabao 48.

1961: Tony Rominger azaliwa
Huyu ni mkali wa kuendesha baiskeli aliyestaafu kutoka Uswisi akishinda michuano ya ‘Vuelta a EspaƱa’ miaka ya 1992, 1993 na 1994 pia alichukua Giro d’Italia mwaka 1995. Alizaliwa mjini Vejle nchini Denmark. Alikuwa mpinzani wa Miguel Indurain katika Tour de France mwaka 1993. Itakumbukwa kwamba mwaka 1994 alivunja rekodi ya dunia mara mbili ndani ya siku chache akitumia saa moja umbali wa kilometa 53.832 na 55.291 kati ya Bordeaux na Velodrome. Alistaafu mwaka 1997 baada ya kuvunjika mfupa (collarbone). Kwa sasa ni wakala wa mchezaji wa Australia, Matthias Brandle.